Alikuwa mwanamke mrembo katika chuo Chao na yeye alilijua hilo,tembea yake na tabasamu lake liliwachanga wanaume wengi na kutaka awe wao
Christina alikuwa toto la kishua,kwao pesa ipo hivyo wanaume wengi domo zege na walala hoi wakawa wanaogopa kumtokea na kuishia kumsindikiza kwa macho anapokatiza na kukwea mringoti kwa mkono mmoja
Siku moja Mama yake Christina alisafiri na kumuacha Binti yake nyumbani, Christina akaona ndio muda wa kujiachia akachukua gari la mama yake na kwenda kupiga nalo misele maeneo mbalimbali ikiwemo chuoni kwao
Bahati mbaya alipata ajali ndogo gari likaharibika,kuepusha shali mama yake akirudi asitambue kitu ilibidi upesi atafute mafundi chuoni hapo anaposoma
Kutokana na namna gari lake lilivyoharibika aliambiwa itachukua muda wa wiki mbili kurekebisha gari lake""wiki mbili zilikuwa nyingi kwa Christina maana mama yake karibu anarudi safari""
Ndipo alipojitokeza moja ya fundi chuoni hapo aitwae Nick moja ya mwanaume ambae huwa anamtamani sana Christina lakini hajui atamuingia kwa gia ipi mtoto huyo wa kishua
Akajikaza akamwambia tatizo la gari lake atalifix kwa muda wa siku chache...hakutaka malipo.. lakini alimuomba bibie amsaidie jambo moja...waigize kama wapenzi chuoni hapo kwa muda wa wiki mbili 😱
Fresh Si Kuigiza tu..na hatufanyi jambo🤔 bibie akaona jambo rahisi kikubwa gari litengenezwe.. akaridhia ombi la Nick
Shida ni kwamba pigo za Nick zilikuwa za kishamba,kutupia code Kali hajui,mwendo na ongea yake vinadhihirisha wazi ni choka mbaya hivyo akawa anamuaibisha bibie chuoni hapo pale walipoonekana pamoja
Bibie akaona siwezi vumilia aibu hizi kwa wiki mbili na huyu Old fashion,akaamua kugharamia akamtoa kwenda kumbadirisha mtindo wake wa nywele,mavazi ya kisasa hali kadharika ongea yake na mitindo mbalimbali ya kishamba aliyokuwa nayo
Inatakiwa Nick afanane kwa kilakitu na bibie,ndani ya muda mfupi baada ya bibie kuingia gharama na kutumia muda wake kumbadirisha Nick nyota yake na uhandsome uliofichwa na shida na ushamba ukaanza kuonekana
Mabinti wengi chuoni hapo wakatamani kuwa nae,Nick alivimba kichwa na kujiona matawi akavunja urafiki na marafiki zake walalahoi,ndani ya muda mfupi akawa star kuliko hata bibie Christina
Akawa hamzingatii tena bibie,kamzowea tayali kwahiyo anataka radha mpya..shida ni kwamba ndani ya muda mchache walioigiza wanatoka pamoja tayali bibie alikuwa kaanza kumpenda Nick serious 😱
Kaonja asali kwahiyo anataka achonge mzinga,Nick sahivi hamzingatii na kumsikiliza Tena bibie yuko bize na marafiki wapya na wanawake wengine,kinyago kakichonga Binti mwenyewe sahivi kinamsumbua
Nini hatima ya penzi lao..
Ni single movie ipo wasiliana nasi
Tags:
movies