HIDAYA NA VICTORIA
_____________________________________
SEHEMU YA KWANZA
Itakuwa poa sana kama ukiniita Hidaya maana jina hili ndilo urithi pekee nilio achiwa na wazazi wangu. Ukiachilia mbali ukoo na kabila langu, mimi ni mzaliwa wa morogoro vijijini ingawaje kabila langu mimi ni muhangaza, maana baba yangu na mama yangu ni wazaliwa wa wilayaya Ngara huko katika mkoa wa Kagera ila upande wangu huko sikuwahi kufika kabisa. Baba yangu alifariki siku ya mimi kumaliza darasa la saba baada ya kugogwa na lori la mafuta, haikupita hata siku mbili mama naye akafuata kwa presha ya kumpoteza mumewe, kuhusu mdogo wangu mimi yeye alifariki zamani sana maana aliliwa na mnyama mkali wakati ameenda kuchanja kuni, na tulichofanikiwa kukipata ni nguo zake zilizokuwa zimelowa damu, basi nikawa nimelelewa na shangazi aliyeko hapahapa morogoro vijijini.Tayari miaka nane imekatika toka niwapoteze wazazi wangu, kwa miaka yote hiyo naishi na shangazi yangu kwa mateso na manyanyaso yasiyo ya kawaida, kutokana na mateso niliyokuwa nikiyapata pale kwa shangazi nilikuwa nikijiona kama mimi ni binti mwenye laana tu maana alikuwa ananitesa isivyo kawaida ni vile siwezi kukuelezea ukanielewa maana inatia simanzi sana, na pia muda haunitoshi maana yapo mengi nahitaji nikueleze yaliyonisibu kabla ya hali hii niliyonayo sasa. Ingawaje nilifaulu ila sekondari niliisikiaga kwa jirani, sikuelekezahata pua yangu, niliambulia mateso na matusi kila siku niwe nimekosea niwe sijakosea yote sawa tena haiwezi kupita siku sijapigwa. Itokee siku moja kwa bahati mbaya binamu zangu watoke shule na wasikute chakula aisee siku hiyo nitapigwa mpaka nizimie. Pale kwa shangazi niliishi kama mtumwa tu maana nayapenda sana maisha yangu. Mapenzi juu ya mdogo wangu ndio yameninifanya niwe hivi maana niliishi kwenye kingo za udailema yani sikuwa nikielewa na wala kujuani wapi naenda, nilienda ilimradi niende tu, hayo maisha ndio yamenifanya niwe hivi. Mdogo wangu aliyekufa kwa kuliwa na mnyama nasi tukafanikiwa kuona nguo zake, kumbe ilikuwepo siri kubwa ambayo hatukuwa tunafahamu, na hata nilipofahamu hapo ndipo maisha yangu yakabadilika na kuwa kama nilivyo leo . Unajuwa nimekuwaje? Tuwe pamoja nikusimulie kisa cha kusisimuwa sana, maana niliyoyapitia kwa hakika ni laana kwangu namajonzi makubwa sihitaji yanikute tena, tafadhali tuwe pamoja mwanzo mpaka mwisho wa life story yangu nitakusimulia ili nawe ukajifunze kwamba binadamu kabla hujafa hujaumbika ndugu yangu, maana unaweza kupitia dhiki kuu leo ila kesho ukaishi maisha ya raha tele au unaweza kumdharau mtu kisa hana kitu leo ila kesho akawa nacho tena wewe ukawa miongoni mwa wanaoomba msada kwake. Ahaaaa! nisikupotezee muda bwana tusonge na haka kastory nilikokuandalia. Kumbuka kametugwa na kuandikwanami Layman Donsue.
SEHEMU YA PILI
Tulipoishia Mapenzi juu ya mdogo wangu ndio yameninifanya niwe hivi maananiliishi kwenye kingo za udailema yani sikuwa nikielewa na wala kujua ni wapi naenda nilienda ilimradi niende, hayo maisha ndio yamenifanya niwe hivi. Mdogo wangu aliyekufa kwa kuliwa na mnyama nasi tukafanikiwa kuona nguo zake, kumbe ilikuwepo siri kubwa ambayo hatukuwa tunafahamu, na hata nilipofahamu hapo ndipo maisha yangu yakabadilika na kuwa kama nilivyo leo Songa nayo...
Basi baada ya kuona pale kwa shangazi naishi maisha ya dhiki na mateso yasiyo ya kawaida, mawazo ya kutoroka yakaanza kupamba moto kichwani kwangu, ingawaje sikujua natorokea wapi na nitafikia wapi ila niliapa kutoroka tuu nikiamini kuwa nikitoroka naweza kupata ahueni huko niendako. Kwa wakati huo nilikuwa na miaka kumi na saba, ila mateso ambayo yamenikuta pale kwa shangazi namzidi mpaka nyanya aliyekula chumvi nyingi (bibi kizee). Pale kijijini nilikuwa na rafiki yangu aliyeitwa Diana huyu ndiye alikuwa mwema kwangu maana asingekuwahuyu mi leo ningeshajiua kudadeki zangu, maana dah! mateso nayo yapitia kwa shangazi sio ya dunia hii, Diana alikuwa wa kunishauri pale napokata tama na kunipa moyo pale nilipo jiona sifai, wazo langu sikuona kama kuna haja ya kumficha, nilimuomba ushauri, aliposikia tu hivyo kwanza aliachia tabasamu kisha akaniambia kuwa nimeamua vyema maana naweza kuishi maisha bila kumtegemea mtu, aliniambia kwamba jioni angenipatia laki mbili ili huko ninakoenda niwe na cha kuanzia maisha, hata kabla hajanipatia nilijikuta nikimshukurusana, ama kweli “akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki”. Kwa hakika huyu naye kwangu alikuwa rafiki mwema sana sikuwa na mwingine wa kumkimbilia maana niliamini kuwa angenishauri ila huyu kanipatia mpaka akiba yake ya mwisho, daah! Msaada wake ulikuwa ni wa hali na mali kwakweli sitamsahau, nilikuwa nikijisemea mwenyewe huku nikirudi nyumbani baada ya kuongea na rafiki yangu. Nilipofika tu nyumbani salamu ya kwanza niliulizwa na shangazi nilikuwa wapi, majibu sina maanatayari alikuwa amenizuia kuwa na mazoea na Diana ila kwangu ilikuwa amri ngumu sana kutekelezwa, kwanza naanzaje kwa mfano maana yule ndiye alikuwa rafiki mwema kwangu, nisingeliweza kabisa kutengana naye. “Wewe kinyago nataka uniambie ulikuwa wapi?” Alikuwa akisema shangazi kwa hasira sana ila mimi cha kumjibu sikukipata kabisa maana ninamfahamu shangazi nikisema nilikuwa kwa Diana mvua ya fimbo inaweza kuninyeshea bila kujitayarisha, nikaona bora nikaekimya huku nikimuangalia kwa hofu kubwa, “Kwahiyo we mbuzi hutaki kujibu sio?, umeanza umalaya wako na yule kinyago wako sio?” Nimjibuje sasa maana malaya mwenyewe anaye zungumziwa ni huyohuyo Diana ambaye ndiye mfariji wangu, sikuwa na cha kumjibu zaidi nilianza kudondosha machozi na kulia nikijiuliza kwa nini Diana anadhalilishwa na kuharibiwa CV yake kwa sababu yangu? Eeh Mungu ipo siku yatakwisha tu lakini, maana hakuna marefu yasiyokuwa na ncha mwisho wa mateso yangu unawadia,one day yes!. “Eeboo! kweli kaka yangu alizaa mbuzi na sio binadamu, kwahiyo wewe ikipita saa hujapigwa unadeka, ona sasa sijakupiga unalia haya unamlilia nani?...lione kwanza”. Alipolitamka jina la baba na kumdhihaki kupitia mimi nilihisi moyo wangu kupasuka nikatamani nimkamate nimvunjevunje ila ndio hivyo uwezo sina maumivu yote nikayamwaga kwa kulia. Looh! kumbe ndio nikawa nimeyakanyaga alinipiga zaidi ya ngoma za makanisani kwenye sifa,baada ya kuambulia kipigo na yeye akiwa amechoka hoi, akaingia ndani na kutoka na nguo nyingi sana eti nizifue na nikimaliza vyombo vinanisubiri baada ya hapo nipike kisha nifanye usafi wa mazingira. Kazi hizo alizipanga na kunitahadharisha eti nusu sa kazi zote ziwe zimeisha la sivyo ananibutua kwa mara nyingine, hata sikujuwa hizo kazi nazifanyaje kwa nusu saa maana nguo tu hazitoshi kuisha ndani ya nusu saa hata ningezifua bila kuzing’arisha, nikabaki kuendelea kulia huku nikifua ili walau nipunguzie adhabu maana nilazimabaada ya hiyo nusu saa napigwa siwezi zifanya kazi zote hizo kwa nusu saa labda ningekuwa na nguvu za kichawi.
Kazi hizo alizipanga na kunitahadharisha eti nusu sa kazizote ziwe zimeisha la sivyo ananibutua kwa mara nyingine, hata sikujuwa hizo kazi nazifanyaje kwa nusu saa maana nguo tu hazitoshi kuisha ndani ya nusu saa hata ningezifua bila kuzing’arisha, nikabaki kuendelea kulia huku nikifua ili walau nipunguzie adhabu maana nilazima baada ya hiyo nusu saa napigwa siwezi zifanya kazi zote hizo kwa nusu saa labda ningekuwa na nguvu za kichawi. Songa nayo.. Wakati naendelea kulia hukunafua zile nguo, mara Diana alikuja na kumkuta shangazi akiwa amenisimamia, shangazi alivyo mnafki utadhani hamchukii dada wa watu yaani alimkaribisha na kumpatia kiti ila yeye akakataa kukaa kwa madai kuwa anawahi, ila kuna kitu tu alikuwa amefuata cha mama yake. Shangazi alivyoingia ndani tu Diana aliingiza mkono mfukoni na kutoa burungutu la pesa na kunipatia kisha kuniasa nitoroke kabla ya nusu saa kuisha kumbe alisikia nilivyokuwa naugulia maumivu wakati napingwa na jinsi shangazi alivyo nipangia kazi nyingi na kunipa mudakidogo wa kuzifanya. Hata kabla sijamshukuru mara shagazi alikuja na kutukatisha mazungumzo yetu kwa kumwambia amekikosa. Ndipo nikaona Diana ametabasamu na kusema eti mama yake alimwambia kama asipo kipata waende naye akamwambie mwenyewe, basi shangazi hakuwa na namna alinisisitiza kuwa baada ya nusu saa hiyo niwe nimemaliza, akirudi akute kazi tayari, kwa kichwa nikaitikia sawa ila moyoni nikasema “urimenya” (kwa wahangaza kule wilaya ya Ngara mkoa wa Kagerawatakuwa wamenielewa kuwa nimemaanisha “utajiju”) kwa maana dah! shangazi nilikuwa namchukia we acha tu, wakati wanaondoka, kwa ishara Diana akaniambia niondoke hiyo ilikuwa gia ya kumtoa shangazi pale ili asinibanebane, nami kwa ishara nikamshukuru sana maana dah kaniokoa kutoka kwenye mikono ya shetani wa duniani. Nilipojihakikishia kuwa tayari wametoka niliingia ndani haraka na kuchukua nguo zangu ambapo baadhi nyingine nikaziacha maana nilikuwa na haraka we acha tu, baadaya kumaliza nilitoka chapu kama mtu ambaye anafuata kitu ili majirani wasije kunihisi kama natoroka. Sikutaka kuharibu hela nilienda kwa mguu mpaka morogoro mjini maana nilikuwa nafahamu njia ambazo zingeniwahisha kufika kule ambapo kwa wakati huo mawazo yangu yote yalikuwa kwamba nikifika stendi nakata tiketi ya kwenda Dar es salaam na siyo kubakia hapo maana niliogopa nisije kamatwa nikarudishwa kwa shangazi yule katili. Mishale ya saa nane na nusu hivi mchana nilikuwa nimefika morogoro nikakata tiketi ya kwendaDar es salaam na kupanda basi, tukawa tumeondoka huku mimi nikiwa na kimuhemuhe cha kutamani kufika ili nilione jiji ambalo nilikuwa nikisikia wanalizungumza sana kuwa ni jiji zuri lenye kuvutia sana jiji ambalo linawapokea watu wote duniani ingawaje wamiliki wa jiji hilo ni Wazaramo. “Sasa nione hao watoto wa shangazi waliodekezwa watafuliwa na nani wakati miaka nane hawajui nguo inafuliwaje na mimi nikiwa mtu pekee ambaye nilikuwa nawafulia, ee Mungu nisaidie huko niendako nisije msahau dada Diana aliyenitoa
kwenye bahari ya mateso” Maneno hayo nilikuwa nikijisemea mwenyewe ndani ya moyo wangu huku nikiendelea kuung’ata ng’ata na kupakata vizuri mfuko wangu ambao nilikuwa nimeweka nguo zangu, maana dah! mateso niliyoyapitia pale kwa shangazi hayakuwa ya kwaida. Usiku wa saa nane nilifika mjini rasmi, huku nikiwa sina mwelekeo matumaini pekee ndiyo yakiwa mwongozo wangu, majumba mazuri na maghorofa marefu yakanipokea mtoto wa watu sina shida, magari ya kifahari yakanikumbusha kuwabinadamu hatu fanani asilani!, wewe ukilala njaa mwenzako vyakula vinabaki na kumwagika, umeme ukanikumbusha kuwa taa za chemli, sola na vibatari au maarufu kama koroboi zinapatika kijijini tu ila siyo mjini, mwangaza wa taa usiku ule ukaniweka bayana kuwa kiza kipo kijijini tu ila mjini kote ni mwanga mtupu, nafsi yangu ikafarijika baada ya kulivua koti langu nililotoka nalo kijijini kwa wingi wa joto mwilini, maana nilikuwa nikisikia tu kuwa huku joto kali ila leo nimejionea mwenyewe.. Looh!Wakati naendelea na ule ushamba wa kushangaa shangaa, ilikuwa ni kufumba na kufumbua nikajikuta mizigo sina na kijimfuko kilichokuwa kimehifadhi hela yangu nacho sina, unajua msomaji nilihisi kuchanganyikiwa kwa sababu vitu nimeshuka navyo vizuri tu kwenye lile basi na nilibaki nimevishika mkononi na hela nilikuwa nimeitunza kwenye mfuko wangu wa sketi ila vyote nimeibiwa nimebakia na sketi na kitisheti nilichokuwa nimevaa tu mpaka lile koti langu nililotoka nalo bushi nililovua baada ya joto kunizidia sikuwa nalo tena.Nikiwa katika yale mawenge ya kuibiwa, mara nilikumbuka kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa ukifika Dar es salaam “abiria chunga mzigo wako” yaani angalia mzigo wako kwa makini, maana unaweza kuibiwa mpaka kiatu ambacho umekivaa mguuni, hapo nikajua tayari nimeshapigwa na kitu kizito yaani nimeshaibiwa. Nilibakia kuduwaa huku nikijiuliza imekuweje ila majibu sikuyapata kabisa, moyo wangu ukajaa maumivu kila nilipojiuliza nitaishije mjini maskini mimi, na njaa isivyo na haya,muda huohuo ikapamba moto tumboni kwangu. Hebu fikiria ndiyo kwanza nimefika, hata sijamjua mtu yeyote pole mjini lakini tayari nimesha ibiwa, maswali kemkem yakajaa kichwa kwangu, kila mtu katika jiji hili alikuwa bize na mambo yake, watu makundi kwa makundi walipishana huku na kule nikabaki mimi na maswahibu yangu nikijiuliza kwanini mimi peke yangu wazazi wangu wote wamefariki, kiza kinene kikatawala fikra zangu, furaha ndogo niliyoipata baada ya kutoka kwa shangazi nayo ikayeyuka kama barafu kwenye jua kali la kiangazi,kwanini mateso yanazidi kuniandama nikiwa bado mtoto mdogo? Kwa nini furaha kwangu ni ndoto? Kwa nini sipati hata siku moja nzima ya kucheka walau mara moja tu?, Kwanini mateso yanione mimi peke yangu? Je nimezaliwa kuteseka tu na wala sio kupata hata chembe ndogo ya furaha? Kama ni mitihani ya maisha ili kutengenza ushuhuda kwanini miaka yote mimi peke yangu? Diana kanisaidia nikatoka kwenye mikono ya shangazi ila badala yakuangukia kwenye mikono salama ndiyo kabisa nimeangukia kubaya zaidi ya nilikotoka.. Aaagh! Kwanini nimezaliwa? Kwanini nateseka na kwanini napitia wakati mgumu kiasi hiki? Naitamani furaha ila furaha imenichukia. Nilikuwa mtu wa kulaumu sana maana wakati ninaoupitia mimi ni kama Mungu naye hanioni, ni kama kanipa mgongo na kunitelekeza nibakie kuteseka mwenyewe kwenye dimbwi la mateso, aaaagh! Masikini mimi.
SEHEMU YA NNE
Tulipoishia... Aaagh! Kwanini nimezaliwa? Kwanini nateseka na kwanini napitia wakati mgumu kiasi hiki? Naitamani furaha ila furaha imenichukia. Nilikuwa mtu wa kulaumu sana maana wakati ninaoupitia mimi ni kama Mungu naye hanioni, ni kamakanipa mgongo na kunitelekeza nibakie kuteseka mwenyewe kwenye dimbwi la mateso, aaaagh! Masikini mimi Songa nayo... Wakati nikiwa kwenye ulimwengu wa mawazo, nikijiuliza maswali mengi sana yasiyokuwa na majibu, nilihisi mtu kanishika begani nami nikawa nimeinua kichwa changu, nilipomtazama huyo mtu aliyenigutusha kwenye mawazo, nikamshuhudia kijana wa makamo kama miaka ishirini na tano hivi.Alikuwa na ndevu kiasi zilizochogwa vizuri, nywele kiasi zilizowekewa dawa nyeusi na kuzifanya zing’ae sana tena zilikuwa zimechogwa vizuri na kupaa kwenda juu, alikuwa na macho madogo kiasi, na pua lake lilikuwa kubwa kiasi kama la wanaume wa kitutsi huko Rwanda, alivaa suti nyeusi na shati jeupe lilokuwa limempendezea sana, alivaa saa ya rangi ya dhahabu huku masikioni alikuwa na earphone ya sikio moja ambayo ilionekana kuwa ilikuwa ikimburudisha kwa mziki, kwa hakika alikuwa kijana mtanashati ambaye toka nimezaliwa sikuwanimewahi kumshuhudia kijana mzuri kama huyo, moyo wangu ulijikuta unakumbwa na hisia fulani ambazo mpaka mimi mwenyewe sikuzielewa kabisa, nimemtamani au nimempenda ama ninamshangaa, sikuwa na majibu zaidi nilibakia kumshangaa tu huku na yeye akiniangalia kwa upole sana, “Habali yako mrembo” Alisema kijana Yule kwa sauti ya upole sana, nilijitazama kwanza nikawa najiuliza hivi kweli mimi ni mrembo ama ananiongopea tu? “Salama tu”Nilijibu ila moyo wangu ukawa unanihukumu kuwa nasema uongo sipo sawa, nami nikawa sitaki kabisa kumwambia shida zangu nikiamini ni kujiaibisha tu na wala hakuna faida yoyote ile, sasa shida ikawa kuudanganya moyo, mwenzenu nikabaki kupambana na nafsi yangu, “Kweli kabisa upo sawa?” Aliuliza kwa mara nyingine tena, hapo nikajikuta kwa haraka nagutuka na kusema “Hapana sipo sawa kabisa”“Pole sana”“Nashukuru kaka yangu” “Nilikuona wakati unashukakatika basi pale stendi ya Magufuli mpaka ulipoibiwa nilikuona pia” “Aliye niibia ulimuona?” “Ndiyo nilimuona ila sikufanikiwa kumkamata ila pole yako” “Aaah! nimesha poa” “Unaitwa nani dada?” “Naitwa Hidaya” “Ohoo mimi naitwa Felix” “Sawa nashukuru kukufahamu, kwanini sasa wewe umenisalimia wakati wengine wote wanapita tu na hekaheka zao wala hawana muda na mimi?”“Kwa sababu wewe ni mgeni wangu” “Mgeni wako?” “Ndiyo Hidaya” Hapo nikabakia kuduwaa na kujiuliza imekuwaje aseme eti mimi ni mgeni wake na wakati tangu nakuja sikuwasiliana na mtu yeyote, ukizingatia kuwa safari yangu hii hakuna ajuaye zaidi ya shosti wangu Diana, lakini zaidi ya hayo yote mimi hapa Dar es Salaam sina ndugu, nipo mimi kama mimi tu. Unajua msomaji nilibaki kuduwaa nikimwangalia kijana huyo,ambaye anasema eti mimi ni mgeni wake ila sikuwa na majibu kabisa badala yake niliendelea kuduwaa tu, kisha kwa mshangao mkubwa nikamuuliza, “Kiaje wewe uwe mwenyeji wangu na wakati sikuwa na ndugu” Kijana huyo alicheka sana kisha Ghafla akanyamanza na kusema, “Unamjua dada yako anayeitwa Victoria yule ambaye mlizika nguo zake na kuomboleza kwa kifo chake?” “Victoria?” Nilihoji kwa mshangao mkubwasana maana Niliposikia jina hilo kwanza nilishituka kisha nikamuangalia sana kijana huyo, maana huyo Victoria alipotea akiwa mdogo sana, na tulipomtafuta tulikutana na nguo yake iliyokuwa imetapakaa damu huku pembeni ya nguo hiyo ikiwepo mifupa ya mtu, tukawa tumeamini ndiye yeye aliliwa na mnyama mkali maana nguo yake ilikuwa imechanikachanika sana, tukawa tumeamini kuwa ni mnyama huyo mkali aliyekuwa ameichanachana kwa kucha na meno yake, sasa leo nakutana na kisamkasa kipya kabisa eti ninaulizwakama ninamjua dada yangu. Nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza ila alikataa akaniambia eti muda wa kumuuliza ukifika ataniambia ila nisikurupuke kumuuliza maswali maana hatoniambia chochote kwa sasa. Je huyo mtu ni nani na amemfahamuje ndugu yang, na ni siri ipi ambayo sijui..
SEHEMU YA TANO
Tulipoishia... Nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza ila alikataa akaniambia eti muda wa kumuuliza ukifika ataniambia ila nisikurupuke kumuuliza maswali maana hatoniambia chochote kwa sasa.Sikuwa na nyongeza nilikubali maana hata hivyo nilikuwa na kimuhemuhe cha kutamani kufahamu mengi sana, maswali nikayapangilia kichwani kwangu na kujisemea ndani ya moyo wangu kuwa atakaponiruhusu tu kumuuliza nitayamimina mwaswali mithili ya mvua ya mawe. Basi alinichukua na kunipeleka kwenye eneo moja walipokuwa wakichoma chipsi akaninunulia chipsi ya kutosha nikara na kushiba sawasawa ili nikimuuliza nisiwe na njaa nimuulize nikiwa na nguvu za shibe, baada ya kula nilipotazamaeneo alipokuwepo yule mtu aliyejitambulisha kuwa anaitwa Felix, hakuwapo tena nikabaki kuduwaa, mara muhudumu wa lile eneo alinifuata na kunipatia simu kisha kuniambia eti amepewa anipatie, nilipouliza chakula kama nimelipiwa akaniambia tayari. Nikabaki kujiuliza kwanza amemtaja mdogo wangu anayeitwa Victoria ambaye alifariki miaka mingi iliyopita hata kabla ya kifo cha wazazi wetu, akaniambia atanijibu maswali yangu ila amenitoroka bila hata kunijibu au angalau kuniaga. Wakati naendelea kujiulizamaswali hayo mara sauti ya mlio wa ujumbe mfupi kuingia katika simu ulisikika, nikaiwasha na kuusoma ujumbe ule ulikuwa umeandikwa hivi, “Toka nje utakutana na usafiri umekungoja na mlango wa gari hilo utakuwa umefunguliwa ili wewe uingie ili uweze kujua kuhusu Victoria dada yako na wala usiogope” Nilinyanyuka nilipokuwa nimeketi, kisha kwenda kutazama huo usafiri ambao umeningoja nje, nilipofika nje mbele ya uso wangu nililiona gari zuri sana ambapo nje ya gari hilo alikuwepo kijana mwingine naye alivaa mavazi kama yule wa kwanzaila huyu alikuwa amevaa na kofia nyeusi, alikuwa amefungua mlango wa gari nami sikuwa na namna nikaenda na kuingia bila kumuongelesha, baada ya mimi kuingia tu mara mlango wa gari ulifungwa, kisha akaenda na kufungua mlango wa mbele na kuwasha gari kisha tukaondoka. Nilibaki nimeduwaa maana kila nilipomuongelesha mtu huyo hakuongea chochote zaidi alibaki kuliongoza gari hilo asiongee chochote kabisa, baada ya muda kama dakika arobaini hivi, tulifika kwenye geti moja kubwa sana lakifahari mara kijana yule akabonyeza rimoti iliyo kuwemo mle ndani ya gari na palepale mlango wa geti ulifunguka na yule kijana akawa ameingiza gari ndani ya geti, tulipoingia ndani nilichokiona mbele yangu kilikuwa cha kushangaza sana yaani naweza kusema ni nusu peponi. Niliona jumba zuri ambalo lilikuwa limepakwa rangi ya dhahabu kiasi kwamba liling’aa kama dhahabu ya Geita. Yule dereva alikuwa wa kwanza kushuka, kisha akafungua mlango wa gari upande wangu, kwa ishara akaonyesha eti nishuke, haponikaamini labda atakuwa ni bubu, ila cha ajabu nikasikia akisema eti yeye siyo bubu kisha akawasha gari na kuondoka zake na geti likafungwa tena, nilibakia kujiuliza imekuwaje ajuwe kuwa mimi namuwaza, na hao ni akina nani na wanahitaji kitu gani kwangu?. Swali ambalo lilikuwa limejipatia kipaumbele kichwani kwangu ni kuhusu mdogo wangu ambaye alifariki miaka mingi sana nyuma, eti leo naambiwa jina lake nikawa najiuliza wamemfahamuje na walijuaje kama mimi nilifika mjini hapo siku hiyo ila majibu sikuyapatakabisa. Wakati naendelea kujiulizia maswali mengi sana mara mlio wa simu kuashilia ujumbe uliingia tena, nikaichukua na kuisoma kwa haraka, iliandikwa hivi, “Kama kweli unatamani kujua siri iliyojificha juu ya mdogo wako anayeitwa Victoria utakachokiona humu usiogope na tukikuruhusu kutoka kwenye nyumba hii utakacho ambiwa usimwambie matu yeyote…Okay! Nadhani umenielewa, sasa waweza kupiga hatua na kuja hapa kwenye huu mlango mkuu wa nyumba utakuta umefunguliwaukiingia subiri maelekezo” Baada ya kusoma ujumbe huo nilipiga hatua na kuusogelea huo mlango, huku nikitamani sana kufahamu yaliyojificha chini ya kapeti, nilipofika mbele ya mlango huo mara ulifunguliwa nikawa nimeingia, nilipoingia tu ndani nilikaribishwa na giza ila giza lilikuwa likipunguziwa makali na mishumaa iliyokuwa imekizunguka chumba chote, mara mlango nao ukafugwa ndiyo kabisa kukawa na mwanga hafifu sana kuliko mwanzo, moyo wangu ulianza kuingiwa na hofu, ila nikajitia ujasiri baada ya kukumbuka ninahitaji kujuakuhusu Victoria mdogo wangu ambaye alifariki miaka mingi nyuma. Wakati nipo pale nasubiri majibu mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu kwa mara nyingine kisha nikaichukua na kuusoma, “Kwa hatua hii sasa unaweza kufahamu siri moja kuwa mdogo wako hakufa, ingia Whatsapp ujue siri kuhusu mdogo wako, kuna video tumekutumia itakayokuonesha jinsi mdogo wako alivyochukuliwa kutoka Morogoro. ”Haraka nilifungua WhatsApp iliyokuwemo mule kwenye simu,nilipoifungua nilikaribishwa na video fupi iliyokuwa ina maelezo machache sana kuitambulisha yaliyo andikwa hivi, “Fahamu ukweli uliojificha juu ya mdogo wako Victoria.” Hayo ndiyo maelezo yaliyo kuwa kwenye ile video fupi. Kila nilipotaka kufungua moyo ulikuwa ukiniruka na kujiuliza kama ni mdogo wangu kweli itakuwaje na wakati kijijini kuna kaburi lake kabisa?, ila baadaye nikaona kadri ninavyochelewa ninapoteza muda tu ikabidi niifungue video ile ili nifahamusiri hiyo ya kwanza kuhusu mdogo wangu wa pekee niliyempenda sana. Nilipoifungua video ile nilikaribishwa na picha ya mdogo wangu, mara nikaona anakimbia, akikimbia kuogopa kitu fulani. Hakufika mbali mara alikamatwa na kuvuliwa nguo zote, kisha wakachukua damu na kuipaka nguo ile na kumbe mifupa walikuwa wamekuja nayo, nikamuona mmoja wao akisema eti waichanechane nguo ile ili ndugu zake na Victoria watakapokuja walaghaiwe akili ya kuwa ameraruriwa na kuliwa na mnyama mkali ndiyo maanawaliiraruararua nguo ile kisha kuiweka pembeni ya mifupa ile, na kumwagamwaga damu pembeni ili ionekane damu zilikuwa zikirukaruka kutoka kwa Viktoria, kwa kusema ukweli nilishangaa sana kuona ulaghai ule uliofanyika. Basi video ile ikawa imeishia hapo. Moyo wangu ulinienda mbio sana, machozi yakaanza kunitoka huku nikijiuliza hao waliomteka Viktoria ni akina nani, na hao ambao wananifuatilia mimi na kunifahamisha kuhusu hili ni akina nani, ila majibu sikuyapata kabisanikabakia kuduwaa na kulia sana.Ujumbe uliingia, kwa mara nyingine haraka nikafungua ujumbe huo na kuusoma.
JE NINI KItaendelea
Full 1000
Tags:
Simulizi