LOVESTORY MOVIES🔞 WAKUBWA TU

Ingia Hapa

Thibitisha Umri Wako

Je wewe ni mpenzi wa simulizi?

Hii ni kwawadau wanaopenda kusoma simulizi bonyeza button hiyo juu kisha chagua aina ya simulizi..

KARIBU KWA HUDUMA KAMA | GRAPHICS DESIGNER | MOVIES NA SERIES FULL HD | HUDUMA ZA MTANDAONI | VIFAA VYA COMPUTER NA MATENGENEZO | VIFAA VYA SIMU NA MATENGENEZO | KUTENGENEZEWA WEBSITE/BLOGS | WASILIANA NASI KUPITIA LIVE CHATI HAPO CHINI AMA TUPIGIE SIMU YA OFISI 0262605123

KAA KARIBU NASI KWA KUJIUNGA KATIKA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPO CHINI

KWA WATEJA WETU WA MBALI LIPIA HUDUMA HAPA NA THIBITISHA MALIPO YAKO NASI TUKUHUDUMIE KWA UAMINIFU MKUBWA
📱JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP

TANGAZA HAPA 🎉CHEZA USHINDE ZAWADI💰

YULE BOY


YULE BOY💓1
Iyo siku ilikua jumamosi bhana, kuanzia asubui sikupata mteja hata mmoja hamuwezi kuamini apo njaa iliniuma kweli kweli, nikatafuta ka chochoro nikapaki gari pembeni, nikawasha redio nisikilize Mechi ya Simba na yanga angalau kidogo itanipooza njaa😁. 

Nikiwa nasikiliza sikiliza mpira kama bahati nikapokea simu ya mteja wangu wa nguvu, yani huyoo mteja anatoa noti nyekundu tu na chenchi unabaki nayo, basi nikafurahi😊 nikapokea haraka. 

"Viki embu nenda pale maeneo ya kinondoni kuna mteja anataka taksi, fanya chap" 

"yupoje yupoje uyo mteja?" 

"Ni mrefu ivii mweusi hata sijui bhana ngoja nakurushia namba yake, changamka basi" Yule Mama akakata simu, haikupita dakika 1 akawa tayari kashanitumia namba ya yule abiria. Chap nikawa nime muwahi mpaka maeneo ya kinondoni nilipo elekezwa. 

Kufika pale nikakutana na bonge la mkaka🥰 nyie ni HB wa maana sana, asikuambie mtu. Nikawa namkodolea macho mpaka alipo zama ndani ya gari. 

"Posta" Mhh sauti ndo usiseme mpaka nikahisi kajoto wakati kilikua kipindi cha mvua mfeew😏, alafu mwenyewe yupo busy na simu yake hataki shobo wala nini sio kama abiria wengine, watakuongelesha mpaka mdomo unauma😄. 

Nikampeleka mpaka maeneo ya posta kuna jengo flanii ivii kubwa sana la vioo nikawa nimemfikisha apo. Kwenye kulipa sasa nikaanza kuona jamaa ana jisachi sachi😅, nikajua hawa ndo wale wale akina Selemani. 

"Bro unanichelewesha aisee!" Nikaweka ngumu, lengo langu anilipe haraka nikale msosi chezea njaa nini! 

"Ahh i don't see my wallet (sioni waleti yangu)" aliendelea kujisachi mwishoni akatoa simu 

"nakutumia hela mpesa ukatoe" 

"mpesa ya nini mzee nipe keshi niondoke maswala ya kutumiwa hela sifanyagi izo shughuli" 

Yule Jamaa akaniangalia sana, akatamani kutabasamu, akawa kajizuia eti akaniwekea sura ya ukauzu labda nitamuogopa😒. 

"unadhani mimi ni tapeli?" nishawaambia tena ana sauti tamu👌 jamani ila kwa njaa zangu nikawa siisikii 

"ilo umesema wewe!" 

"okay subiri hapa namtuma mtu akuletee" Akaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya lile jengo nikasema wee usinitanie yaani uniache hapa alafu unikimbie? Nilimsogelea na kumnyang'anya simu yake, alishtuka na kunigeukia akiwa kachukia sana😡 

"unadhani mimi ni tapeli? ok subiri unaletewa hela yako" akaingia ndani. 

Ile simu yake ilikua iphone 15 weee😅, nikashangaa, kamoyo kakaanza kunisuta kwa kutomuamini kaka wa watu. Mda sio mrefu mlinzi alitoka na hela akanipa kisha akachukua simu ya Bosi wake na kuondoka nayo. Jamaa alinipa elfu 50 badala ya elfu 25 mhhh🤔. 

Nikasema labda kakosea kuhesabu, Nani arudishe? Nilichomoka lile eneo spidi kama sio mimi niliekua nadai hela😁. 

Kwa majina naitwa Victoria Simon, mwenyewe napenda kujiita Viki. Mimi ni yatima sina baba wala mama😔. Mpaka nakua nilikua nalelewa kwenye kituo cha watoto yatima. Nilikaa sana pale mpaka nikaona Nitoroke na mimi nikajitafutie maisha ndo nikaja kudondokea kwenye 
u-dereva teksi. 

Hii kazi ina ugumu nyie acheni tu, Maana ma dereva wa kiume wananitenga mnoo, nikienda kijiweni wana nifukuza kwaiyo unakuta mafuta yangu yana ishia kwenye kuranda randa na sio kubeba abiria. 

SONGA NAYO.... 

Lile Gari mimi nimelikodisha na kila wiki namlipa jamaa hela, sasa ikawa hadi imepita miezi miwili sijamlipa saa ngapi asije kuchukua gari lake😭. Nikawa nalala tu nyumbani nikiwaza napata wapi hela. 

Pale ninapoishi nakaa na wadada wawili mmoja anaitwa Salome mwingine Debora, wao kazi yao kubwa ni kudanga, pesa wanapata kweli na maisha yao ni mazuri.
Wakawa wana nishauri na mimi nijiunge nao. 

"Twende leo basi ukajionee, kwa usiku mmoja hauwezi kosa chini ya laki 7, embu fikiria kwa siku mbili utakua na shingapi?" 

"Kweli Viki tena wewe ni karembo, tukimpa Baba Dangotee atakupa hata milioni" Debora akawa ana msapoti Salome. 

"kweli?" kusikia milioni masikio yakanisimama kama Nipashe nikawaza nikubali au nikatae?🤔 

Akubali au akatae??? Nini kitaendelea???

Full 1000

YULE BOY 💓2

TULIPOISHIA........ 

"Twende leo basi ukajionee, kwa usiku mmoja hauwezi kosa chini ya laki 7, embu fikiria kwa siku mbili utakua na shingapi?" 

"Kweli Viki tena wewe ni karembo, tukimpa Baba Dangotee atakupa hata milioni" Debora akawa ana msapoti Salome. 

"kweli?" kusikia milioni masikio yakanisimama kama Nipashe nikawaza nikubali au nikatae?🤔 

TUENDELEEE......... 

Kichwa kikaanza kupata moto, nikaona bora niende nikadange mara moja, nikipata hela naenda kuikomboa taksi yangu nirudi mzigoni.

"sawa nitaenda" 😔 

"woyoooooo ayo ndo maneno sasa, ulikua una sita sita nini?" Salome alifurahi, akaingia chumbani kwake akatoka na magauni manne, akanirushia nichague. 

"nitavaa hili" nilichagua gauni ambalo halinichori sana 

"weee nawe acha ushamba, vaa hili, hata kama hauna shepu kama sisi hili litakufaa sana" Debora alisema kweli, Sikua na shepu ila sura sasa ni🔥. 

Wenzangu walifurahi ila mimi sasa nilikua nime nyong'onyea sana mpaka tunafika sehemu yenyewe sikua na hamu🥺. 

Kuna Baa moja kubwa sana ilikua imefunguliwa maeneo ya Mbezi Beach, uko sasa watu wenye hela zao ndo wana burudisha moyo. Debora na Salome tayari walisha ongea na uyoo Baba Dangote kwaiyo tulivyo fika tu pale tukaja kupokelewa na walinzi wake tukapelekwa mpaka alipokua. 

"woooow Dangote mwenyewe, Mtu wa mipesaaa" Salome akaanza kukashobokea kale kazee😅, nyie yani kazee kama kale kanashindwa kukaa nyumbani na mkewe kanakuja kutafuta vidada usiku usiku. 

"Mamaaa Salome naona umeniletea sukari, alafu bado mbichi kabisaa" Nilimkata jicho yule kizee nikatamani nimchambe nikaona bora nifunge mdomo wangu nisije kosa hela. 

"sogea huku na wewe" Salome akanivutia kwa kale kazee, Nikajikuta nimekaa kwenye mapaja yake😔. 

"sisi tunaenda, Binti mwenyewe ndo huyoo kazi kwako Dangote" 

"haaha! Ok, mlinzi wangu atawapa chochote na nyie mka enjoy" Kizee kina sifa kama nini😒 

"Asante Dangoteeee" Debora na Salome wakasema kwa pamoja utadhani hawajahi kuona hela kabla. 

Basi walipoondoka nikawa nimebaki na kile kizee apo natetemeka hatari. Kizee chenyewe kikawa kinanisifia mara aniambie utajiri wake angejua tu jinsi alivyo nikera bora angefunga mdomo wake😒. 

"twende basi tukapumzike eeeh mrembo" Mimi naitikia tu kwa kichwa, kimoyo moyo naomba Mungu kale kazee kasije kaka nigusa uwiiiiii😭 maana bado nilikua bikra🙈. 

Kabla hatuja nyanyuka pale kale kazee kakapokea simu ya dharura kwaiyo nikawa nime ponea kwa staili iyo, ila aliniachia kiasi cha laki 5🥳, Nikashukuru Mungu sana siku iyo. 

Siku iliyofuata nikaenda kumlipa yule jamaa akanipa taksi nikarudi zangu barabarani! Mda huo nilikua nisha sahau kabisa kuhusu yule kaka HB  nilikua nawaza kazi tu. 

Sasa siku moja jioni, nikiwa maeneo ya Posta saa ngapi gari lisinizimikie? 🙆‍♀️ alafu sasa mfukoni sikua hata na senti tano maana nilitoka kuweka mafuta mda sio mrefu. 

Simu nayo haikua na salio nyiee, ukisikia siku ya kufa nyani miti yote huteleza ndo hii sasa. Ikabidi nikae pembeni nichekeche akili chap chap juu ya nini nifanye. 

"Why are you here ( kwanini upo hapa?)" ilikua ni sauti traaamu👌 iliyo nisemesha ikabidi nigeuke ndo nikakutana na suraa ya mwamba tena kawa kauzu balaa sijui kama anachekaga. 

"sikuelewi mimi" 😂 

"Nauliza kwanini upo hapa?" 

"Ai bro usinifokee bhana, gari langu limezima" 

Jamaa akasogea mpaka kwenye gari🚘 akaliangalia angalia kisha akarudi mpaka pale nilipokua nimekaa. 

"Namtuma mechanic wangu aje alifate, in the mean time twende niku drop nyumbani ni usiku sasa ivi" 

"nitaenda mwenyewe" si unajua tena nyodo nyodo ili nibembelezwe😂 

"okay, kesho ulifate gari lako ofisini" 
Jamaa ni mkavu huyuu hata hakunibembeleza, aliingia zake kwenye gari lake na kuondoka, nikawa siamini kama nimeachwa pale! Sasa nitarudije nyumbani😭. 

Kwa mbali mvua nayo ikawa inataka kunyesha🥺, jamani nikakoma kuweka mapozi ya ajabu kwa watu ambao hawana utani. 

Nikachukua boda boda mpaka nyumbani, nikakuta Debora na Salome ndo wanataka kutoka, wakanikopesha hela nikamlipa yule boda lasivyo sijui ingekuaje🤦‍♀️. 

"Heee ndo kilicho kukuta? Makubwa yani naisi uyo kaka hamshindi Baby wangu kwa ukauzu" mimi na Debora tukashangaa kumbe Salome ana mpenzi! 

"yani una mpenzi na sijui" Debora akabaki mdomo wazi 

"yeah ninae, Ndo ana nipa hela za matumizi, unafikiri kupendeza huku ni hela za kudanga tu?" 

"Sasa kama una mpenzi kwanini unadanga? Si utulie tu ufanye biashara au utafute kazi!" Nikatoa ushauri ambao Salome alicheka😂 mpaka basi. 

"kudanga kuko kwenye damu, alafu mimi nishazoea kupata hela za chap chap maswala ya kusubiri mwisho wa mwezi siwezi au kuingia hasara kila siku sababu biashara haiendi? No!" 

"kwaiyo shemu anajua unadanga?" 

"hajui chochote, Kwanza hata sijawai kulala nae, nimemwambia mpaka ndoa, kama hataki apite ivii sina mda wa kubembeleza mtoto wa mtu" 

"aiseee Salomeee shikamoo! Tutambulishe basi tumjue!" Nikamsapoti Debora na wazo lake. 

"hapana! mtamuona siku ya harusi! sitaki mumuone, nampenda sana!" 

Yani Salome ni waajabu sana, anapata mtu wa kumpenda alafu analeta leta nyodo je sisi ambao hatuonekani?😂 japo salome alitukatalia kutuonyesha jamaa wake ila kiukweli nilitamani sana kumjua maana alimsifia mpaka kero😔

Je jamaa mwenyewe ni nani??? 

Full 1000

YULE BOY💓3

TULIPOSIHIA... 

"hajui chochote, Kwanza hata sijawai kulala nae, nimemwambia mpaka ndoa, kama hataki apite ivii sina mda wa kubembeleza mtoto wa mtu" 

"aiseee Salomeee shikamoo! Tutambulishe basi tumjue!" Nikamsapoti Debora na wazo lake. 

"hapana! mtamuona siku ya harusi! sitaki mumuone, nampenda sana!" 

Yani Salome ni waajabu sana, anapata mtu wa kumpenda alafu analeta leta nyodo je sisi ambao hatuonekani?😂 kusema kweli nilitamani kumjua huyo shem Darling maana siyo kwa misifa ile.....

TUENDELEE...... 

Salome hakuwa tayari kututambulisha tuliachana naye hatukutaka kumlazimisha🤣🤣🤣nililala zangu wao wakaondoka kwenye mishe zao.....kulipokucha....

Kesho yake asubui na mapema nikaenda ofisini kwa yule kaka, nikakuta kweli gari langu lipo pale sema sasa wakagoma kunipa eti mpaka Bosi wao aje😒. 

Nikasema isiwe kesi nikakaa pale nje nikamsubiri aje, kweli mda sio mrefu akawa kafika. 

Jamaa aliposhuka tu kwenye gari lake, akanipita kama hanioni nyie😂, nikashangaa kwani ana matatizo gani? Kwaiyo ukinisaidia kidogo tu ndo uni nyanyase? 

Nikamfata nyuma mpaka tukaingia ndani ya ule mjengo. Kumbe ile ilikua ni Kampuni ya Mitindo, kuna modo wa kila aina, kila saizi unaipata! 

Watu kule ndani wakawa wananishangaa😳 namfata Bosi wao nyuma nyuma na hanifanyi chochote. 

"come in (ingia ndani)" akanambia baada ya kufika ofisini kwake sasa mimi na kingereza ni maji na mafuta nikawa nimeganda tu mlangoni. 

"ingia!" apo ndo nikawa nime muelewa. 

"Bro! asante kwa kunisaidia, nimelifata gari langu sasa" 

"ok" akanijibu kifupi huku akichezea pc💻 yake, Nikaona zarau zimekua nyingi nikatoka zangu nikaendelee na mishe mishe. 

Majira ya mchana Akanipigia simu nimfate ofisini kwake, sijui namba yangu alitoa wapi ila cha kushangaza zaidi jamaa ana gari na dereva juu lakini anaishia kupanda taksi🤔. 

Nikamfata mpaka ofisini kwake nikamkuta yupo nje ananisubiri 

"Bro kabla hujaingia, hakikisha kwanza kama una hela mfukoni, sitaki tukifika uko uanze kujisachi sachi" nilikua nipo seriazi kweli, nikamuona anatabasamu😊, aiseeee kuona tabasamu lake moyo wangu uka suuzika sijui kwanini! 

"Heee kumbe una tabasamu? Wooow" nikamsogelea karibu nimuangalie labda naota, alipoona namshangaa sana akarudisha sura ya ukauzu. 

"ukimaliza kushangaa, utanikuta ndani ya gari" 

"wee nawe unani kata stimu sasa😔😔😔!" Niliwasha gari tukaondoka lile eneo nikampeleka kwenye hoteli flani ivii alikua ana kikao mchana ule😒😒😒. 

"nisubiri mpaka kikao kiishe😐😐😐!" 

"Aah nikipata mteja je🤔🤔🤔? Aaah hapana! Fanya ivii ukimaliza kikao nipigie nikufate" 

"subiri mpaka nimalize kikao✋️✋️!" alishuka kwenye gari akaondoka.  

Nikasema ni sawa  hata ivyo hakua amenilipa,nikaona bora nimsubiri tu mpaka amalize kikao atanilipa mara tatu yake😒😒. 

Nimekaa pale kama lisaa nikaona mhudumu kaja na chakula kikiwa kimefungwa pamoja na soda eti kapewa aniletee🤣🤣😋. 

Na hivi sikula tangu asubuhi, nikaanza kukipiga pale pale😁😁😁, kilikua ni chipsi na mazaga zaga kibao. 

Kama unavyo jua mpendwa baada ya kushiba sana nini kinafata? Tena mimi nashikwaga na usingizi mzito ile mbaya😑😑😑.
Nikashusha kiti, nikajilaza zangu vizuri, haikuchukua mda sana usingizi💤 ukawa umenipitia. 

Nikatandika usingizi kwa mda mrefu, na ivi nilikua na kauchovu uchovu basi nililala kama nimekufa. Nakuja kushtuka tayari giza limeingia na jamaa kashatoka kwenye kikao saa nyingi, na kasha sepa. 

Nilichukia iyo siku sitakaa nisahau😔😔😔. Yani namsubiria mtu alafu anaondoka na kuniacha😡. Nilipo waeleza Salome na Debora wakanicheka hatari. 

"ndo ukome unalala sana" 

"pole mwaya shoga angu achana na salome! Kwakua unapajua ofisini kwake basi kesho mfate asubui😔😔😔" 

"Kesho mapema atanikuta mlangoni kwake nilijisemea hivyo na kusonya mijitu mingine bwana😒😒😒, mda wote huo niliokua nimelala nisinge kosa wateja zaidi ya wawili" bado roho iliniuma hatari😁. 

"hivi Viki huchoki kua taksi dreva kila mtu ana kudharau🙄🙄🙄? Achana na hio kazi haikufai hata kidogo, kwanza Baba Dangote ana kutaka, yupo tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa😍😍!" 

"Salome, embu muache mwenzako! Kashasema hataki ni hataki✋️✋️" 

"Sitaki ukweli, kwanza ile siku ilikua ni bahati mbaya tu, na kale kazee jinsi ambavyo sikapendi ninaweza hata nikakanyongea usingizini mimi!" niliondoka kwa hasira😡 nikawaacha wananishangaa. 

Wazee kama hao walinikera mno, tena ndo chanzo cha watoto wengine kua yatima😭. 

Siku iliyofuata nikajiandaa chap chap, nikawa wa kwanza kufika ofisini kwa yule jamaa hata sijui anaitwa nani! Nikamsubiriii weeeee mpaka nikachokaa, nikakaa kila staili mwishowe nikapata wazo la kuingia ndani kumuulizia. 

Sekretari wake akanipokea vizuri hana makuu dada wa watu ila akanambia jamaa siku hio haji ofisini😑😑😑😔. 

"kama una namba zake mpigie, maana Bosi kanambia leo na kesho hata kuja ofisini, atafanyia kazi nyumbani" 

"Namba zake hata siku zisevu, kwani ana kaa wapi?" 

"hilo siwezi kukuambia maana ni kinyume na utaratibu wa kazi, labda urudi jumatatu" 

"Haaaaaaa jumatatu mbali maana namdai"😁 

"una mdai?" mpaka sekretari akashangaa😳 

Tukiwa tunaongea mara akaja dereva wa jamaa alikua katumwa baadhi ya mafaili ampelekee nyumbani kwake, nikasema hapa hapa, lazima nimfate nyuma nyuma nijue wapi alipo, hawezi kukimbia bila kunilipa😂.

Je viki atafanikiwa kupajua nyumbani kwa Jamaa??? Unahisi nini kitafuata???

Full 1000

YULE BOY💓4

TULIPOISHIA........

"hilo siwezi kukuambia maana ni kinyume na utaratibu wa kazi, labda urudi jumatatu" 

"Haaaaaaa jumatatu mbali maana namdai"😁 

"una mdai?" mpaka sekretari akashangaa😳 

Tukiwa tunaongea mara akaja dereva wa jamaa alikua katumwa baadhi ya mafaili ampelekee nyumbani kwake, nikasema hapa hapa, lazima nimfate nyuma nyuma nijue wapi alipo, hawezi kukimbia bila kunilipa😂.

TUENDELEEE...... 
 Yule Dereva baada ya kuchukua vitu alivyoagizwa aliondoka nami fasta🤣🤣🤣nikaanza kumfatilia  nyuma nyuma mpaka nikachoka maana alisimama karibia kila sehemu, mara supamaketi mara drai klina, mara hotelini mpaka nikasikia hasira na ukiangalia kengele ishaanza kulia kuashiria gari halina mafuta. 

Safari ikawa inaendelea nikiomba Mungu gari lisizime uwii mbona itakua kimbembe🙆‍♀️. Mwishoni yule dereva akasimama nje ya bonge moja la mjumba, ni mkali uo hatariii🔥. 

Nikapaki gari langu pembeni nikaenda kubisha hodi, akaja iko kimlinzi kina mashauzi utadhani kinafanya kazi benki mfeew😔😒☹. 

"Kama huna apointimenti na bosi hapa huingiii✋️" 

"Ivi unajikuta nani😏😏? unafikiri ningetoka huko kote nije mpaka huku bila kuitwaa🙄🙄? Embu acha wazimu nifungulie niingie😑😑" 

"we niletee mdomo😐😐, mimi ni kama bosi hapa nikiamua vilevile hutaingia✋️✋️" Alivuta simu📱 akapiga mahali, Alipomaliza geti likafunguliwa nikaruhusiwa kuingia. 

Nikawa najiuliza mbona nimeruhusiwa kuingia ki ulaini kumbe jamaa alikua ananiona kupitia kamera za getini😆😆😆. 

"vipi tunadaiana😐😐?" Nikaulizwa swali nikiwa mlangoni hata ndani sikuingia 🤔🤔

"Kwaiyo unajifanya hujui ulicho kifanya? Nipe changu niondoke🧐🧐" 

"Nilikuambia unisubiri sio ulale😎😎!" 

"Nipe changu bhana sitaki maelezo mengi😣" 

"okay twende ukachukue🫤🫤" Aliingia ndani na mimi  nikamfuata💃💃. 

Ndani kwake ni pazuri💋💋👌, mwanaume yupo vizuri kweli, kuanzia mpangilio, usafi, urembo na kaharufu kataamu🙈🙈. 

Sasa akanipeleka mpaka jikoni, mimi nikawa sielewi iyo hela ambayo iko jikoni ni ipi😹😹? 

"listen, Nina wageni mda sio mrefu, na wanapenda sana kula🥱🥱🥱, please if you can naomba, uwapikie, nitakulipa kiasi chochote" Duuh kumbe ana jua kuomba😕😕🤣 

"Mimi nimefata hela yangu sijafata kupika😉😉, alafu kwanza wewe ni mrushi kweli sikuamini hata kidogo😒😒😒" 

"Nitakulipa laki mbili🤨🤨" 

"laki mbili?" 😳 

"Haitoshi? Laki tatu🥴🥴!" 

Kusikia Vile nikakubali mwenyewe kiulainii kabisaa kwani kupika shi ngapi bhana😫😫😫. Dada enu nikaanza shamra shamra za mapishi mda huo jamaa alikua sebuleni, alafu nilisahau kumuuliza hata jina lake🤣. 

Mtoto wa kike nikaanza kukarangiza mpaka jamaa akajileta mwenyewe jikoni😁😁😁, mi napika yeye kakaa pembeni ananiangalia😆😆😆, aibu ikanishika hatari🙈. 

Nimemaliza kupika pale, nikaandaa misosi mezani, matunda matunda na vikoro koro vya kila aina. 

"Nice!" nikasifiwa pale😁 nusu nisahau kama namdai 

"unaweza kusubiri mpaka wageni watakapo ondoka?" 

"Mhhh! Bro nimechoka hatari, nilipe tu niondoke!" 

"Nitakulipa mpaka wageni watakapo ondoka!" 

"ivi wewe mkaka una nini lakini mbona unataka kunipelekesha? Ujuwe nina kazi zangu!"☹ 

"Nitakulipa" alielekea chumbani kwake akaniacha nikiwa najiuliza🤔 mbona anapenda kunizungusha zungusha sana🤔🤔. 

Basi ikanibidi nisubiri mpaka atakapo malizana na wageni wake🥲🥲🥲. Kwenye Kusubiri saa ngapi usingizi usinipitie? Weee nilala kama gogo 🤣. 

Jamaa alipokuja kuniangalia akakuta nimelala💤, akanibeba akanipeleka chumba cha wageni, akanifunika vizuri na blanketi, mwenzenu nakoroma sina habari khaaa huu usingizi jamani mbona unapenda kuniaibisha🥲🥲

Mbuzi kafia kwa muuza supu😁😁😁nini kitaendelea???

Full 1000

YULE BOY💓5

TULIPOISHIA... 

Basi ikanibidi nisubiri mpaka atakapo malizana na wageni wake. Kwenye Kusubiri saa ngapi usingizi usinipitie? Weee nilala kama gogo 🤣. 

Jamaa alipokuja kuniangalia akakuta nimelala💤, akanibeba akanipeleka chumba cha wageni, akanifunika vizuri na blanketi, mwenzenu nakoroma sina habari usingizi nao kwa kuniaibisha lol😔😔😔

TUENDELEE..... 

Tangu hiyo jioni niliposhikwa usingizi nikaja shituka usiku mida kama ya saa 8 hivi😔😔😌nikaanza vuta kumbukumbu mmmhh nikaamka nikawaza usiku huu nikamwamshe kweli😆😆😆si ataniona mchawi vyema niwe mstaraabu hadi pakuche duh nililala Palipokucha asubui nikaamka nikatandika kitanda😔😔

Ila mimi jamani, nilikuja kudai hela yangu na sio kulala kwenye nyumba za watu😬😬, aibu gani hizi😫. 

Nilitandika kitanda vizuri nikapanga panga nilipomaliza nikatoka, nakuta jamaa kaandaa breakfast hiyoo ni hatari kweli kweli😪😪😪. 

"Good Morning (Habari za asubuhi)" 

Huyu naye kwa kizungu nikabaki kimya tu😔

Habari ya asubuhi😦😦ilibidi arudie kwa kiswahili

Nikajibu

"salama!" 

" sit (kaa)" nikakaribishwa mezani, mimi ni nani nikatae mapocho pocho ya asubui?🤣 

"Viki, Wageni walipenda sana chakula chako, nimefikiria nikuajiri kama mpishi wangu endapo ukikubali, trust me nitakulipa vizuri sana!" 

"unajua jina langu?" Kati ya yote aliyo sema sikuyafurahia kama alivyo taja jina langu🥰 

"yes" 

"lakini mimi sijui jina lako" 

"unakula na unalala kwa mtu ambae hujui ana itwa nan🥴🥴🥴 you are not serious" 

"Mda wote una kunja sura tu unafikiria nitataka kujua jina lako saa ngapi"🤨😕 

"Kweli?" Jamaa alicheka 😅, nikaona meno yake yalivyo meupee🤣 😁 

"Daaah ungekua unacheka ivyo kila siku ungependeza sana🙈🙈" 

"i know, Sio kila mtu ananiona nikicheka😺, ni watu wachache sana! Kwa chakula chako nimefanikiwa ku saini Mkataba wa pesa nyingi mno, ndo maana nina furaha! By The way jina langu ni Carrick" 

"Sawa Mr Carrick" 

"Umekubali kua mpishi wangu?" 

"naomba mda kwanza nifikirie" 

"okay" 

Carrick alinipa pesa zangu kidogo kamoyo kakasuuzika😊, nikarudi nyumbani kwa raha tele. Lile ombi la kua mpishi wake ikabidi niwashirikishe Debora na Salome ili wanishauri🙈🙈. 

Waliniambia nikubali tu maana ukiangalia kazi ya taksi hainilipi sana kama nilivyo tegemea, kwa sababu hio nikakubali kua mpishi👩‍🍳 wa Carrick. Nikawa naenda asubui na kurudi jioni. 

Sasa siku moja nilichelewa kutoka kwa Carrick na jamaa alivyo hana huruma akanambia niende nyumbani na anaona kabisa mda umeenda😖😕. 

Nilinuna vibaya mno ila sikua na jinsi maana Bosi mwenyewe haeleweki mara akuchekee mara akukazie sura🥹🥹 . 

Wakati nawai kituoni, mara mvua ikaanza kunyesha na sikua na mwamvuli😭, aisee nilitukana matusi ya kila aina. Kumbe Carrick alinifata nyuma, nashangaa nafunikwa na mwamvuli🥰. 

"ukitukana sana ndo mvua itakata au😳😳?" 

"Achana na ilo hujaja na gari🥺🥺?" 

"sijaona funguo🫤🫤!" 

"sawa hujaona funguo ndo uje na mwamvuli☂️ mmoja? Yani hapa tunanyeshewa tu" 

"neno asante linakushinda kusema? je nisinge kuja kabisa? Twende turudi😧😧" 

Nikarudi na Carrick mpaka kwake ila yeye alikua kaloa hatari😁😁😁, mimi ndo nilikua mkavu. Akawa ana piga chafya huku ana tetemeka🥶, yani akinyeshewa tu kidogo lazima apate homa, na mimi sikua najua ilo. 

Nikaanza kumhudumia pale usiku mzima mpaka homa ikawa imeshuka na mimi nikapitiwa na usingizi💤 nikiwa chumbani kwake, nikaona nilale pale pale kitandani kwake karibu yake, Duuh bora nisinge fanya vile🥺. 

"weweee! Amka amka amka! Fanya haraka!" Nyie nyie asubui Carick si akaniamsha kama mwizi🤨🤨? Namkuta kapandwa na hasira utadhani sio yeye alienifata jana usiku mvua ikiwa inanyesha. 

"kuna nini?" hata sielewi chochote niko zangu bize nafikicha fikicha macho 🤣🤣🤣

"nani kakutuma ulale hapa? Nakuuliza nani kaku ruhusu ulale kitandani kwangu?" 😡 

"jamani Carrick jana ulizidiwa ikabidi nikuhudumie ndo kwa bahati mbaya nikapitiwa na usingizi"

"Mimi kuumwa kidogo ukaamua kutumia nafasi ya kujitongozesha? Au ulifikiria nini, labda nakupenda kwakua nilikufata na mvua😨😨? Hivi nyie wanawake mkoje?" Aisee maneno ya Carrick yaliniuma hatari mpaka machozi yakawa yana nilenga lenga🥺 

"Nilicho fanya ni kukusaidia tu, sijaona kama kuna ulazima wa wewe kunitolea maneno machafu kama hayo🥹🥹🥹" 

"usinge taka maneno machafu unge jiheshimu sio kufanya ujinga ulioufanya, toka chumbani kwangu, Tokaaaa" 🗣 

Lol nilinyong'onyea😔😔😔 nikaanza kuondoka chumbani kwake....

Je nini kitafuata???? 

Full 1000
kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Previous Post Next Post