LOVESTORY MOVIES🔞 WAKUBWA TU

Ingia Hapa

Thibitisha Umri Wako

Je wewe ni mpenzi wa simulizi?

Hii ni kwawadau wanaopenda kusoma simulizi bonyeza button hiyo juu kisha chagua aina ya simulizi..

KARIBU KWA HUDUMA KAMA | GRAPHICS DESIGNER | MOVIES NA SERIES FULL HD | HUDUMA ZA MTANDAONI | VIFAA VYA COMPUTER NA MATENGENEZO | VIFAA VYA SIMU NA MATENGENEZO | KUTENGENEZEWA WEBSITE/BLOGS | WASILIANA NASI KUPITIA LIVE CHATI HAPO CHINI AMA TUPIGIE SIMU YA OFISI 0262605123

KAA KARIBU NASI KWA KUJIUNGA KATIKA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPO CHINI

KWA WATEJA WETU WA MBALI LIPIA HUDUMA HAPA NA THIBITISHA MALIPO YAKO NASI TUKUHUDUMIE KWA UAMINIFU MKUBWA
📱JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP

TANGAZA HAPA 🎉CHEZA USHINDE ZAWADI💰

FUMBO LA NDOA

UTUNZI WA RIWAYA: FUMBO LA NDOA
MTUNZI: JUSTIN BARUTI
MWAKA: 2024/2025
WHATSAPP: 0752474397
UTANGULIZI

Kila mwanamke anaingia kwenye ndoa akiwa na ndoto za furaha, amani na upendo. Katika baadhi ya jamii ndoa sio tu hatua ya kimaisha bali ni matarajio makubwa yanayotegemewa na familia, jamii na kila mwanamke mwenyewe. Lakini je, ni kwanini baadhi ya wanawake uishi maisha ya majuto huku wengine wakiwa na furaha?

Katika simulizi hii ya Justin Baruti tutaingia ndani ya safari ya ndoa kupitia macho ya Mariam, mwanamke aliyekutana na changamoto ambazo wanawake wengi hawajui kabla ya kusema *ndio*

Fuata simulizi hili ili kuelewa fumbo hili lenye siri kubwa

*SEHEMU YA 1*

Alikuwepo binti mmoja kijijini Mugumu jina lake Mariam alikuwa na umri wa miaka 25, binti mrembo mwenye ndoto kubwa za maisha bora ndani ya ndoa. Kijiji hiki kilijulikana kwa jamii yake inayopenda sherehe za harusi na matarajio makubwa kutoka kwa wanawake wa kijiji icho. Mariam alitamani sana siku moja kuolewa, kuanza safari ya maisha ya pamoja na mpenzi aliyekuwa na heshima na upendo

Lakini safari ya ndoa sio rahisi kama ilivyotazamwa na wengi au wengi wanavyodhani. Mariam alijua hilo vema akijitayarisha kwa mawazo mbalimbali akijiuliza mara kwa mara ni kwa nini wanawake wengi uishi maisha ya majuto baada ya ndoa? Je, ndoto zake za maisha bora ndani ya ndoa zingeweza kufanikishwa?

Mariam alikua na ndoto za mpenzi ambae angesimama nae wakijenga maisha ya pamoja kwa furaha na upendo. Ndoto za ndoa kwake zilikuwa za amani, familia yenye furaha na watoto waliobarikiwa lakini mara nyingi mambo hayaendi kama alivyoyategemea

Siku moja wakati kijiji kizima kikiandaa sherehe za harusi kwa shauku, Baruti mwanaume maarufu kwa heshima yake kijijini alifika nyumbani kwao Mariam akiwa na zawadi za kawaida ikiwemo unga wa mahindi na sukari lakini hata hivyo kusudi lake halikuwa hili bali alitokea kumpenda Mariam kwa moyo wake wote, taratibu alianza kumtongoza

“Mariam umekua sasa nahisi wakati umefika” alisema Baruti kwa sauti nyororo

Mariam alimuangalia kwa tahadhari kwa upendo alikuwa nao lakini bado hakuwa na uhakika kama Baruti ndie mtu sahihi wa maisha yake aliyekuwa akimtafutia maisha bora

Alikumbuka maneno ya mama yake aliyekuwa amekwisha dhihirisha matarajio ya kijiji kwamba ndoa lazima ifanyike.. akamtafuta mama yake

“Mama kwanini unaamini kwamba Baruti ndie chaguo bora” aliuliza kwa sauti ya chini akiwa na hofu

“Mariam sio tu kuhusu Baruti, ni kuhusu heshima yako kama mwanamke. Maisha ya kijiji hiki yanakutegemea uolewe mapema na mtu mwema” mama yake alijibu akiwa na hakika

**************************

Baada ya mashauriano mengi Baruti na Mariam walifunga ndoa. Sherehe ilikuwa ya kifahari kijijini kila mtu alishangilia mwanzo mpya wa familia hiyo lakini ndani ya moyo wa Mariam kulikuwa na maswali mengi ambayo hakuwa na majibu nayo

Ndoa yao ilianza kwa furaha ya kawaida. Baruti alikuwa ni kijana mkarimu na mpole lakini muda ulivyopita katika ndoa yao changamoto ziliibuka polepole. Baruti alikuwa mtu wa kazi sana mara nyingi hakuwa nyumbani na mke wake, Mariam alijikuta akiwa mpweke na watoto wadogo aliowapata ndani ya ndoa hiyo

Anapojaribu kueleza hisia zake kwa Baruti mwanaume huyo hakuwa na wakati wa kumuelewa na alipokuwa akisikitika Baruti, aliona kila kitu kiko sawa huku akijitahidi kupata chakula cha familia na kuendesha maisha ya kawaida

Mariam alikumbwa na upweke na ghafla alihisi kama alikuwa amekwama katika maisha ambayo si yake. Upendo ambao alitarajia haukuja vile alivyofikiria na matarajio ya ndoa kama kisiwa cha amani yalionekana kufifia

Alikumbuka mashairi aliyosoma akiwa mtoto ambapo wanawake waliimba kuhusu ndoa kuwa sehemu ya furaha ya milele lakini sasa Mariam alikuwa na hisia za kutofautisha

“Ndoa sio tu kuhusu kuolewa bali ni kuhusu kupata mpenzi anayekuelewa” Mariam alijitafakari akiwa peke yake usiku huo..

Sehemu inayofuata itakuwa na changamoto mpya za fumbo ambalo linahitaji kufumbuliwa. Fuatilia ili kuelewa

(USIKOSE SEHEMU YA 2) Nunua Simulizi hii Nzuri Ya kusisimua full kwa shilingi 2000 tu.

Nunua hapa👇

Lipia na Thibitisha

Previous Post Next Post