Baada ya mama yake RIZVAN KHAN kufariki Dunia RIZVAN aliamua kusafiri kutoka nchini kwao India kwenda kuishi kwa kaka yake nchini Marekani
RIZVAN hakuwa vizuri sana kiakili alikuwa kama chizi flani Lakini anajielewa kama MEMO wa kwenye miracle in cell sio kama ROHIT MEHRA🤣
Baada ya kufika nchini Marekani alikuwa akimsaidia biashara kaka yake ya uuzaji wa vipodozi maeneo mbalimbali nchini Marekani
Siku Moja katika mishe zake hizo alikutana na na bibie MANDRA/KAJOL katika saloon anayofanyia kazi, taratibu wakajenga mazowea final wakafall in love na kufunga ndoa licha ya tofauti zao za kidini
RIZVAN alikuwa muislamu na MANDRA alikuwa muhindu,pia ana mtoto kwajina la SAMEER aliyempata katika mahusiano yake ya awali,licha haya yote na uzezeta wa RIZVAN waliishi kwa furaha
Penzi lao liliingia dosari siku ambayo OSAMA BIN LADEN alipolipua majengo mawili marefu nchini humo na kusababaisha mauwaji ya watu wengi
Hali hii ilipelekea waislamu wote kuonekana ni magaidi,hivyo waislamu wakaanza kukutana na vikwazo vingi kama kukosa ajira,kuishi kwa woga,kutengwa na biashara zao kuyumba
Ugomvi huo ulipelekea SAMEER mtoto wa MANDRA kufariki baada ya kushambuliwa na vijana watukutu wa kizungu
Hali hii ilimuuma na kumkasirisha sana MANDRA huku akilaumu ndoa yake na huyo muislam RIZVAN KHAN ndio imechochea kifo Cha mwanae
Kuanzia muda huo mapenzi yakapungua hakutaka kumuona tena RIZVAN na kumtaka aondoke nyumbani kwake na kumwambia ili urudi hapa iambie Dunia kwamba wewe sio gaidi
Akampa wakati mgumu RIZVAN kwa kumwambia afike mpaka kwa Rais wa Marekani kumwambia kwamba MY NAME IS KHAN I'M NOT A TERRORIST Kisha urudi
Utamu wa movie ni namna RIZVAN anavyokutana na vikwazo mbali mbali akiwa njiani kuelekea kwa Mr president
Ni single movie, tunayo Whatsapp na telegram sh 1000
link ya kutupata hii hapa Download Movie hii hapa
Tags
movies