DOWNLOAD BURE MOVIES ZA WAKUBWA TU

Ingia Hapa

Ingiza Password

Je wewe ni mpenzi wa simulizi?

Hii ni kwawadau wanaopenda kusoma simulizi bonyeza button hiyo juu kisha chagua aina ya simulizi..

KARIBU KWA HUDUMA KAMA | GRAPHICS DESIGNER | MOVIES NA SERIES FULL HD | HUDUMA ZA MTANDAONI | VIFAA VYA COMPUTER NA MATENGENEZO | VIFAA VYA SIMU NA MATENGENEZO | KUTENGENEZEWA WEBSITE/BLOGS | WASILIANA NASI KUPITIA LIVE CHATI HAPO CHINI AMA TUPIGIE SIMU YA OFISI 0262605123

KAA KARIBU NASI KWA KUJIUNGA KATIKA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPO CHINI

KWA WATEJA WETU WA MBALI LIPIA HUDUMA HAPA NA THIBITISHA MALIPO YAKO NASI TUKUHUDUMIE KWA UAMINIFU MKUBWA
📱JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP

TANGAZA HAPA 🎉CHEZA USHINDE ZAWADI💰

NDANI YA GETI

NDANI YA GETI 1 - 6
Sehemu ya 01 na 02

Sehemu ya 01
Vijana wawili Said na Abiola walikuwa wanakatiza katika mitaa ya Madale Mkoroshini ambapo walikuwa nyuma ya mtoto wa kike aliyekuwa anatembea mwendo wa maringo huku mkononi akiwa ameshikilia mfuko uliojaa viungo vya chakula maana alitoka sokoni

Sikioni alijiwekea Earphones za Apple huku akisikiliza kawimbo taratibu

"Zakia ee, Zakiiii" Aliita Abiola ambaye alikuwa nyuma kidogo ya binti huyo

Hata hivyo kutokana na binti kuvalia Earphones, ilipelekea kutosikia pindi anaitwa hivyo hakuitika

"Mfuate, acha uoga" Alisema Said huku akimsukuma Abiola aweze kumuwahi binti yule

Abiola alijikaza kisabuni na kumfuata mtoto wa kike, ukweli moyoni ni kwamba alikuwa anaogopa sana si unajua mtoto wa kiume kwa msichana mpaka amuanze basi inakuwa ni ngumu sana

Abiola alienda mpaka binti alipokuwa anatembea...ndipo akaanza kumtazama kwa ukaribu huku kijasho chembamba kikimtoka

Zakia alimuangalia kuanzia juu mpaka chini kwa dharau, halafu alisimama na kutoa earphone kwenye sikio moja na kuguna "Mh" Alisema huku akibetua mdomo wake

"Zaki Mambo?" Aliuliza

"Safi" Binti alijibu huku akizidi kumkagua yule kijana

"Poa tu, nakuita muda wote lakini hunisikii sijui ni kwa sababu ya earphones zako hizo?" aliuliza

"Ndio, embu nieleze shida yako"

"Zaki, unajua kabisa nilishakuambia muda mrefu kwamba nakuhitaji sana, sasa inakuwaje unanikatili, message hujibu lakini"

"Heee" Binti alitoa sauti ya mshangao "Hivi nikuulize swali Abiola?"

"Niulize"

"Mara ngapi nimekuambia kwamba mimi sikutaki sikutaki sikutaki!!!! Siwezi kuwa na mwanaume kama wewe naomba uniache"

"Samahani lak...."

"Lakini nini? Nishasema sikutaki, wewe unavyonitazama hivi mimi ni hadhi yako? Embu angalia watu wa hadhi yako huko..." Alisema mtoto wa kike na kisonya mfyuuuu halafu akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka haraka

"Dah" Abiola alichoka, alibaki akimshangaa

Huku nyuma Said alikuwa amechuchumaa anakufa mbavu kwa kicheko, yaani alicheka sana hasa pale alipokumbuka mshikaji wake anamtambiaga kwamba mwanamke yule anampenda sana

"Daaah!" Alisema Side

"Nini sasa?" Abiola aliuliza

"Man, yaani huyu demu mdogo sana unamshindwa mtu una kazi kabisa unalipwa mshahara laki 6 huyu demu unamshindwa?"

"Aaagh mapenzi sio pesa mtu wangu, ila mapenzi ni kwamba demu akupende mwenyewe, mi huyu demu nakuambia ni mgumu hata ukihonga milioni hatokubali" alisisitiza Abiola

"Acha ufala"

"Ufala gani? nakuambia kwamba ni hivi hata wewe ukomae vipi huwezi mpata huyu demu" Alisema kijana huyo

"Mimi? mimi kabisa Side mimi au Side mwingine?" Aliuliza Said

"Wewe hapo ndio"

"Tuwekeane Dau" alisema jamaa huku akinyosha kidole cha mwisho ili wapinge

"Ok....ukimpata huyu demu nakupa laki moja Side"

"Laki????" aliuliza kwa mshangao

"Yah laki moja, yaani ukishindwa laki unanipa mimi"

"Haina noma, nielekeze anapoishi niende"

"Nakupeleka mwenyewe"

"Poa twende"

Side na Abiola walikuwa vijana watani sana, hivyo walitembea wakibishana njiani ili akaonyeshwe sehemu binti alipokuwa akiishi.

Walifika maeneo yaitwayo Panga Boy ambapo pale pangaboy kulikuwa na nyumba nyingi za kifahari zilizojengwa na matajiri waliokuwa wakiishi mitaa hiyo

Vijana hao walifika katika eneo lenye nyumba moja ya kifahari ya ghorofa Moja, iliyokuwa nyeupe na ilikuwa imezungukwa na ukuta mweupe vile vile

Ukuta ulie ulikutanishwa na geti Jeusi la kisasa na la bei kubwa halisi, pembeni kulikuwa na switch ya kupigia kengele ili ufunguliwe vile vile kulikuwa na kamera ilikuwa ikimulika nje

"Ndo wapi sasa?" Side aliuliza

"Ni hapa" Abiola alisema huku akinyoosha mkono kwenye geti

"Ni wa kishua hivi?" Aliuliza

"Yah, ila yule ni mfanyakazi wa ndani tu, katika nyumba hii, hivyo basi nakuachia jukumu la kumtega ndani ya geti hili"

"Mh" Side aliguna kwa uoga uliojaa mshangao....ITAENDELEA
Sehemu ya 02
Kesho yake asubuhi Side aliamka mapema sana, hii ni kwa sababu Side alikuwa na tenda ya kwenda Kariakoo kwa ajili ya kuchukua mzigo wa viatu vya kike ambavyo mara nyingi alikuwa akifanya kuvitembeza mtaani ili apate chochote kitu cha kuendesha maisha yake mjini hapo.

Hata hivyo alipofika kule aliweza kukutana na muuzaji wake wa kila siku alichukua mzigo wa kutosha kisha akapanda gari ya Tegeta Nyuki halafu akamalizia na Bajaji ya Madale mwisho ambapo yeye alishuka mkoroshini.

Kijana huyu alikuwa akiishi Maeneo ya hapo hapo Mkoroshini. 

Side kichwani mwake hakuwa na kumbukumbu ya upuuzi wowote ila alipanga kabisa

"Leo, naenda mpaka Mbopo nataka nikauze huko" Aliwaza peke yake na kuupanga mzigo vizuri kisha akatia begi mgongoni na baadhi ya viatu akashika mkononi na kutoka nje akafunga mlango

Kijana huyu alikuwa machachari sana, mwenye maneno matamu ya kuvutia wateja kila alipopita, hata hivyo alitembea haraka haraka maana hakutaka jua kali limkute njiani

Akiwa anatembea kwa bahati mbaya au nzuri njia ya kwenda Mbopo ilipita pale pangaboy pakiwa ni center.

Alipofika tu alishtuka na kukumbuka lile tukio alilokuwa ameambiwa na Abiola jana yake, kijana Side alitabasamu na kutembea mpaka karibu na nyumba ile.

Hata hivyo alifika karibia na geti lile akasita kidogo na kuogopa huku akiwaza asije akawa alipelekwa sehemu ambayo siyo, mwisho wa siku akakutana na shida tupu huko.

Side alitazama kushoto kulia ndipo alipomuona mzee mmoja akipalilia mahindi, hivyo akasogea karibu yake na kumpa salamu

"Hallo habari?" Alimsalimia

"Salama hujambo"

"Sijambo mzee wangu naona unaendelea na majukumu"

"Ndio ili watoto wale bwana si unajua?" Alisema mzee huyo alivaa kibarakashia kichwani

"Ni kweli, samahani mzee wangu kwenye hilo geti eti ni kwa nani?" Aliuliza Side

"Hapo bwana ni kwa mtu mmoja anaitwa mpemba" alisema mzee huyo

"Anaonekana ana pesa eh" aliuliza Side na kusogea karibu "Lakini samahani kuna binti namsaka, nasikia anaishi humu anaitwa Zakia" Aliuliza

"Hahahaa....Zakia maharage ya Mbeya?" alisema mzee huyo side akashtuka kidogo 

"Anaitwa Maharage ya Mbeya?"

"Ndio, yule binti mteremko sana kila mtu anapiga tu"mzee alionekana muhuni sana yule

"Duh" Side alicheka sana maana yeye ndo alichokuwa anakitaka hicho kichwani aliwaza kwamba laki si kashaipata ile kirahiiisi, dooh...."Huyo huyo ndo namtaka mzee wangu" Alisema Side na kutabasamu.

"Haya njoo simama hapa" Mzee alisema hilo suala

Side alimsogelea na wote wakawa wanatazama getini mule

"Ndani ya hilo geti jeusi kuna vitu humo" alisema mzee "Mizigo kweli kweli"
 
"Wacha"

"Ndani ya geti hilo kuna Mnazi...chini ukiingia utakuta mama mwenye nyumba chini ya mnazi ameketi anapanga majukumu ni mwarabu mama huyo"

"Ehee"

"Kushoto na kulia, mbele na nyuma amezungukwa na wanawake wa aina mbalimbali wa nne, kila mmoja ana umbo lake mzee, mmoja wao ni huyo Zakia halafu kuna watoto wadogo wa kiume wanacheza si unajua likizo hii?" Alisema mzee

"Ndio ndio"

"Juu ghorofani upande wa nyuma kule kuna Ua....nipe buku hapo" Alisema mzee akinyoosha mkono kumbe maelezo yote yale alikuwa kazini mwamba huyo

"Hahaaaa" Side alizamisha mkono mfukoni akatoka na buku buku kama sita hivi, akamtolea hapo moja na kumkabidhi "Nikiingia kuna bifu??"

"Hamna huyo mama anacheka cheka tu" Mzee alisema na kuweka jembe begani akaondoka zake huku akimuacha Side njia panda

Side alijiuliza sana atawezaje kuingia ndipo mwisho akapata jibu anaingia kama muuza viatu mule ndani aone kama atafanikiwa akishindwa basi bwana.

Side alipiga hatua, moja, mbili, tatu, nne, tano mpaka kumi akafika getini na kugusa switch ya kengele. Akasikia huko ndani krrrrr trrrrrring.....huko ndani ya geti moyo ukampiga paaah.

Aliogopa akatamani kuingia ndipo akasikia geti limefunguliwa kutazama hivi ni mtoto mdogo kabisa wa kiume aliyekuwa ameshikilia filimbi mkono wa kushoto

"Shikamoo"

"Marahaba, samahani nitamkuta nani huku?" Side aliuliza

"Mama" alijibu mvulana huyo

Mtaalam aliingia ndani ya geti huku akiogopa ogopa, mkononi akishikilia viatu ndo vilikuwa mtetezi wake ili akiulizwa kilichomleta basi ajibu kwamba anauza viatu.

Hata hivyo mtaalam alipofika ndani kijana yule mdogo alirudishia geti lake na ndipo mtaalam alipotazama ndani.

Kiukweli, kila alichokuwa ameambiwa na yule mzee kama vile alikikuta. Maana alishangaa anakutana na wanawake wanne wa nguvu, wakiwa wanafanya usafi mule ndani.

Mmoja aliyekuwa wa umri wa kati ya miaka 28 hadi 30, alikuwa ameinama anafua nguo

Wa pili aliyekuwa na miaka kati ya 23 mpaka 25, alikuwa anapalilia maua

Wa tatu alikuwa ni Zakia, ambaye alikuwa akifagia fagia pale chini kwa chelewa, alikuwa amevaa kwa nidhamu nguo iliyofika pale mguuni, halafu alimgeuzia macho Side huku akirembua

Wa nne alikuwa bonge la mmama, mwenye miaka kati ya 38 hadi 40, alikuwa mnene mwenye makalio makubwa na alikuwa akifuta vio huku akiwa amepanda juu ya stuli

"Dooooh" Alisema jamaa, huku udenda ukimtoka kwa kila mwanamke aliyekuwa anamtazama pale ndani.

Side alikodoa macho mbele kama vile yule mzee alitabiri, yaani mama wa kiarabu kabisa alikuwa ameketi chini ya mnazi bila kuogopa kudondokewa na nazi kutoka juu mama huyo alikuwa akitabasamu huku akijitikisa tikisa na kuchezea simu yake.

Side alisalimia "Jamani habari za asubuhi" Alisema lakini hakuna hata mmoja aliyeitikia ila walimgeukia mama boss wao kwanza

"Shikamoo mama" Aliamkia side ndipo bi mkubwa akainua macho na kumtazama

"Marahaba" Alisema mamaa huyo

Side alisogea karibu na mama yule akamuomba radhi "Samahani mama nimeingia katika himaya yako, mimi ni mfanya biashara nauza viatu kwa kutembeza katika nyumba za watu, kama utahitaji unaweza ukaniungisha" alisema

Mama mwarabu alimtazama tu bila kujibu chochote ndipo akapata jibu kwamba yule mama hana utani. Ghafla mtaalam alisikia kitu kimemdondokea kichwani, akashtuka sana na kupeleka mkono kichwani akakitoa hicho kitu, yaani alipokitoa tu hivi alitazama akakuta ni ganga la ndizi mbivu

Watu wote pale ndani walicheka ikabidi jamaa ainue uso kutazama juu ghorofani, ili ajue nani aliyemdondoshea lile ganda.

Kitendo cha kuinua uso hivi tu, kidogo kijana huyo angezimia, hakuamini kiukweli pale juu ghorofani kulikuwa na mtoto mrembo, aliyekuwa anacheka baada ya kudondosha ganda lile alicheka sana


Side na binti huyo waligongana uso kwa uso yeye na mtoto huyo ambaye alikuwa mzuri mnoooo mwenye asili ya kipemba, yaani Mwarabu sio mwarabu, Mpare sio mpare, muhaya sio muhaya, mchaga sio mchaga, mnyakyusa sio mnyakyusa, mmasai sio mmasai, mbulu sio mbulu, mzaramo sio mzaramo, mbena sio mbena muha sio muha.

Unywele mrefu ulishuka mpaka hapa mgongoni halafu alikuwa ana macho makali na pua ndefu kidogo. Yani hadi  mtaalam alidondosha kifurushi cha viatu akawa anamshangaa.

Halafu mtoto huyo alimnyooshea mkono kwa ishara ya kumuita...Side akabaki mdomo wazi

Moyoni alitamani amfuate ila alimuogopa mama yake akahisi sio vyema anaweza akajitafutia matatizo.

Mbaya zaidi alishasahau kilichomleta ni kumtafuta Zakia ili apate laki moja.....ITAENDELEA
NDANI YA GETI 
Sehemu ya 03 na 04
Sehemu ya 03
Tuliishia pale Side alipokuwa akiitwa na mtoto mkali juu ya Ghorofa akawa anahofia mama yake.

ENDELEA SASA
Side alibaki ameduwaa, macho ameyainua juu anamtazama malaika huyo aliyeonyesha ana miaka kati ya 18 mpaka 20 pekee.

"Mungu wangu huyu ni mtu ama???" Alijiuliza kwa mshangao halafu akakumbuka maneno ya yule mzee pale nje ya geti ambayo yalisema hivi
*"Juu ghorofani upande wa nyuma kule kuna Ua....nipe buku hapo" Alisema mzee akinyoosha mkono kumbe maelezo yote yale alikuwa kazini mwamba huyo*

Unajua kijana alishangaa sana maana aligundua Ua alilokuwa anaambiwa sio ua mmea bali ni ua binadamu

"Doooh......opppps" Alivuta pumzi watu wakabaki wamemshangaa.

"Sasa si uje, nakuita muda wote unaogopa nini?" ilitoka sauti kinanda juu ghorofani, Side mwenyewe aliogopa. Alimgeukia maza na kumtazama kwa jicho lililotoa maelezo kwamba niende au nisiende? lakini mama yule alicheka tu kama ilivyokuwa kawaida yake

"Kijana wangu" Mama wa Kipemba aliita

"Naam mamaa" Side aliitika kwa nidhamu

"Nenda kamsikilize mwanangu huko juu, huenda ikawa anahitaji viatu" Alisema mama huyo kwa kujiamini lakini bado Side aliogopa

"Enh?" Aliuliza

"Nenda ukamsikilize mwanangu" Alisema mama.

Kwa uoga Side aliinama na kuokota viatu alivyokuwa amedondosha chini halafu akainuka na kumtazama mama ambaye muda wote alikuwa anamtazama Side

"ngazi zipo upande gani?" Side aliuliza

"Zunguka hivi" Mama alielekeza kwa mikono na Side akatembea kwa uoga sana kuelekea pande hizo alizoambiwa zina ngazi.

Akilini mwake alihofia sana, alihisi labda wanataka kumfanyia kitu, lakini kiume alijitia nguvu na moyo "Ngoja niende, liwalo na liwe" alijisemea na kuanza kupanda ngazi

Mtaalamu alipanda mpaka ghorofani pale akamkuta binti anamsubiri huku akiziweka nywele zake vizuri ndipo alipompa salam

"Salam Alaikyum" alisema side

"Walaikum Assalam...mbona muoga hivi?" Aliuliza yule binti

Side alitabasamu na kufuta jasho halafu akaweka mzigo chini "Hamna sio uoga, hizi nyumba mpaka CCTV camera, mh hatuziamini" Alisema

"Usijali, kuna kiatu chekundu nimeona umeshika kiko wapi?" Aliuliza binti huyo

Side alikagua katika mzigo ule na kuvitoa viatu vyekundu jozi mbili "kipi kati ya hivi?" Aliuliza

"Hiki" Binti alisema na kuchagua kimoja akakichukua na kuanza kukikagua kikampendeza sana "Wow, hiki kizuri sana, ni sh ngapi?" aliuliza

"Hicho nipe 22 tu nakuachia dadaaa" Alisema mtaalam akianza kuyazoea mazingira

"Halafu wewe" Binti aliongea "Usitaje bei kubwa kwa kuwa unaniona katika nyumba nzuri hivi taja bei ya ukweli usinionee"

"Mh hiyo ndo bei hiyo kwani we unanipa shilingi ngapi?" Aliuliza

"ntakupa 20" alisema binti yaani alishuka elfu mbili pekee

"Dooh, utakuwa umeniua but sawa toa hela yako"

Ghafla walisikia sauti ya mama kule chini "Nuru....!!!" mama alifoka na yule binti aligeuza uso akiangalia chini mama alipokuwa 

"Abee" Alisema

"Muda umeisha, aondoke mi sitaki kesi na baba yako" Alifoka sana mama huyo

"Mh yaani hawa" Binti alizungimza kwa hasira halafu akatoka pale na kufungua chumba ndipo akatoa na noti mbili za elfu kumi kumi na kumkabidhi Side, yaani hata kujipima kiatu hajajipima, kiatu chenyewe side kanunua 6000 kule Kariakoo yaani alifurahi mno

"Asante sana dada yangu" Alisema side

"Usijali, uwe unapita mara moja moja huku kwetu maana huwa hamuingiagi humu kabisa"

Side alitabasamu "Usijali tutakuja" Alisema 

Alikusanya kila kilicho chake akashuka ghorofani na kuaga halafu akaondoka mazima.

Side alifika nje ya geti hakuamini, Alichanganyikiwa na alisimama getini huku akiwaza sana

"Yaani kumbe ndani ya hili geti kuna ua lisilo la kawaida? Daaah, yaani ningempata yule demu ningemlamba mwili mzimaa mamayeee" Alisema kijana huyo kwa kujiamini "Ni hatari sanaaaa.....ila kuwapata hawa wapemba ni kisangaaa" Alijikatia tamaa kijana huyo halafu akaondoka

Kijana side alikuwa na oda za viatu kwa baadhi ya watu huko Mbopo vivyo alijitahidi kupeleka ili awasambazie.. Lakini pia pesa aliyokuwa ameingiza kule ghorofani ni nyingi kwa maisha ya mtanzania, hakika ni shida. Alipagawa na mtoto wa kipemba.

Jioni jioni Alifunga biashara yake akarudisha vitu nyumbani kisha akaoga na kutembea kijiweni. Alimkuta Abiola mshikaji wake wa karibu sana akiwa anakula muhindi wa kuchoma, akampa tano na kuketi

Abiola alivunja muhindi na kumpatia Side halafu wakaanza story

Side: Mzee baba naomba namba ya Zakia jana nilisahau kuichukua

Abiola: Dooh, nishafuta man

Side: Aaah sasa mbona unazingua man

Abiola: Sijazingua fanya mchakato uakaichukue mwenyewe, tena ndo itakuwa rahisi kumtongoza, sio aanze kukuuliza namba kakupa nani

Side: Sio mbaya, nakuaminia boss
*
Kichwani mwa Side alikuwa anataka amuonyeshe Abiola kwamba yeye ni kidume, lakini sasa hata alipofika kule kwa kina Zakia hakuweza kuongea naye badala yake alimtamani binti mwingine kabisa....ITAENDELEA

Sehemu ya 04
Kila mara side alikuwa akicheka hasa alipokumbuka yule mzee alimwambia kwamba Zakia anaitwa Maharage ya Mbeya

"Sasa maharage ya mbeya ndo amemsumbua mshikaji wangu hivi jamani?" Alijiuliza akiwa amelala kitandani
BAADA YA SIKU TANO
Side alikuwa katika harakati zake maeneo ya Flamingo, mji karibu kabisa na Madale ambapo mtaalam aliingia mtaa mmoja kulikuwa na soko mjinga akiwa anatembeza viatu mdogo mdogo. Hata hivyo kwa mbali aliona gari nyeupe ikitokea katika chocho moja ndipo mwamba akasimama na kuipisha ile gari asijegongwa bure

Gari ile ilipaki mbele yake na dereva alishusha kioo akamtazama kijana usoni

"Habari yako kijana?" Aliuliza dereva

"Fresh Fresh" Alisema Side na kumsikiliza kwa makini

"Ebwana samahani sana, mi naelekea sehemu moja inaitwa Mkoroshini, sasa sielewi ni wapi embu nielekeze"

"Aah broo, nipatie lift naenda huko huko tukifika ntakuonyesha"

"Mia" Dereva alifungua mlango na jamaa akazama ndani ya gari huku akipaka begi la viatu vyake.

Ilikuwa ni majira ya saa 10 jioni, walitembea kwa mwendo wa haraka kidogo, wakafika Mkoroshini

"Hapa ndo mkoroshini" alisema jamaa hivyo dereva akapaki gari 

"Ahaa, poa mzee ngoja nimpigie mtu fulani anipokee"

"Poa" Mshikaji alifungua mlango na kushuka, ila kabla hajarudishia mlango hivi alisikia kasauti ka jamaa kakisema

"Niko mkoroshini.....eeh njia ya Mbopo ni ipi tena?.....ok niulizie mbopo halafu Nashuke pangaboy? Haya poa" alisema dereva huyo ikabidi Side amsaidie

"Kwani unaelekea wapi we braza?"

"kuna mzee mmoja ameniajiri katika kampuni yake sasa ameniambia nikamchukue mtoto wake nimpeleke mjini mara moja, anaishi maeneo sijui Mboko sijui Pangaboy yaani kanichosha kishenzi"

"Anaitwa nani huyo mzee"

"Halifani ila wengi wanamuita Mpemba mwenye asili ya kiarabu hivi"

"Mpemba??" Said aliuliza kwa mshtuko

"Yah vipi unamfahamu?"

"Broo nakupeleka hadi home, usinilipe hata mia mamaee....." Alisema kwa furaha kijana Side na kukwea ndani ya ndinga Ilikuwa furaha isiyo ya kifani kila alipokumbuka kuna Ua kula ndani ya geti alitamani hata akalitazame tu

Walianza safari yeye kazi yake kumuelekeza tu

"Bro, mimi usinishushe nje ya geti, nataka uniingize mpaka ndani ya geti kuna demu mkali mule ndani broo ni mzuri kudadekiiii nikamuone tu"

"Haina noma....nafikiri ndo huyo ninayeenda kumchukua"

"Man, ni wa kiarabu eti"

"Hahahaa....twenzetu"

Waliongea mpaka wakafika nje ya geti.

Dereva alipiga honi sana, ndipo Side akaona akamsaidie akashuka na kubinya kengele kikalia ndani. Kabla hajarudi kwenye gari, geti lilifunguliwa, na alipotazama hivi ni kile kisura mtoto malaika hasaa.

"Mambo jamani" Side alisema kwa furaha huku akimnyooshea mkono wasalimiane

Kwa dharau yule demu alimtazama juu mpaka chini huku akimkagua kama vile hawakuwahi kuonana kabla, Side aliishiwa pozi

Kabinti kalifungua geti kubwa gari ikazama na jamaa akaisindikiza nyuma

Siku hiyo hakukuta mtu nje, siku hiyo kulikuwa patulivu kabisa ila TV iliimba Qaswida ndani ya nyumba.

"Samahani mimi naitwa Isaac nimetumwa hapa....." alisema Dereva lakini kabla hajamaliza sentensi mtoto wa kike alizima

"Alright baba amepiga simu tuna taarifa ngoja kwanza nikamuage"

"Ok"

Binti yule aliingia ndani na kumfuata mama yake "Mama, ndo kafika yule kijana mi naondoka"

"Sawa, ila mwambie baba yako muwahi kurudi"

"Sawa" 

Huku nje Dereva Isaac na Side kama vile walizoeana haraka mno, walikuwa wakicheka ndani ya gari

"Daah kademu kenyewe katakuwa ndo haka" alisema Isaac

"Ndio kenyewe yaani man....kananikosha sana rohoo"

Gafla mtoto alitokea ikabidi waizime ile mada

"Kaa siti ya nyuma mzee baba" Alisema Dereva na Side bila kusita alishuka na mabegi yake akahamia siti ya nyuma

Mtoto wa kike alipofika pale alisita "Unaitwa Nuru bila shaka" Aliuliza 

"Yes" Alijibu kwa kifupi ndipo akasogea mlango wa nyuma akaufungua

"siti ya mbele ipo mdogo wangu" alisema Isaac

"Hapana ntakaa huku nyuma"

"Ok"

Nuru alizama ndani na kuketi pembeni mwa Side, moyo ukamdunda ti ti ti, Alichanganyikiwa aliona anavyoenda kuzalilika ila jina ashalijua ni Nuru 

Safari ya kurudi nyuma ilianza wakatoka nje ya geti halafu wakaanza kutembea mdogo mdogo kuelekea mkoroshini

"Daah" Side aliwaza "Naanzaje sasa?" alizuga huku akiwa anaangalia mbali, ingekuwa ana smartphone basi angeitoa mfukoni azuge nayo

Safari ilisogea kimya kikatawala, Isaac akawasha Muziki...hapo kidogo ikampa confidence Side kwa kujua hata akijibiwa vibaya basi jamaa hatosikia

😂Wanaume wana taabu😅

"Nuru" Side aliita kwa sauti ya upole na ya kinyenyekevu, lakini binti akamgeukia bila kuitika "Pale ni kwenu?" Aliuliza swali la kizushi la kuanzia

Nuru hakumjibu, aliangalia juu chini kama mara tatu hivi halafu akatoa simu aina ya iPhone akaanza kuchezea.

Side aliishiwa nguvu, akatulia na jasho likavuja japo AC ipo ndani ya gari.

Baada ya hapo, side aliingiza mkono mfukoni na kutoa Wallet kama mtu mweye pesa sana, halafu akaifungua ndani kulikuwa na vikaratasi vidogo vidogo vingi kinyama

Alichomoa hapo kamoja na kumnyooshea binti, bila hiyana Nuru alikipokea na kukisoma kilikuwa kina namba za simu kumbe huyu mwamba ana tabia ya kuweka namba za simu kwenye wallet ili akikutana na manzi ampatie kirahisi 😂😂

Nuru alicheka halafu akakichana chana na kukitupa kupitia dirishani kwa dharau....ITAENDELEA
NDANI YA GETI 05 N
Sehemu ya 05

"Mh" side aliguna, ujanja wote mfukoni "Sasa mbona unanifanyia hivyo jamani?" Alisema mtaalam

"nini?"

"Basi nipe no yako tutachat"

"Hahaha...." Binti alicheka huku akiziba mdomo wake kwa kiganja "Namba yangu kirahisi rahisi hivyo? Huna hadhi ya kuwa na namba hii" Alisema mwanamke huyo jamaa akabaki mdomo wazi aliyejikatia tamaa

Hakuweza kuongea tena. Jasho lilimtoka akaogopa na kusinyaa.

Walifika mkoroshini "Broo niache hapo" Alisema

Isaac alisimamisha gari na jamaa akashuka huku akiwa ameumia moyoni sana kwa kukaziwa na mtoto wa kike

*

Gari ilikuwa ikielekea mjini Alikuwa Isaac na Nuru pekee ndani ya gari lao na binti alikuwa siti ya nyuma huku mtaalam akiendesha

Isaac mwenyewe aliutamani ule mwanga pale ndani na alizima muziki akaanza kuongea naye

"Nuru" Alisema jamaa huku akitazama kwenye kioo maalumu kilichokuwa kikionyesha kinachoendelea siti za nyuma

"Abee" Binti aliitika huku akiacha kuitazama simu ndipo alipoinua macho na kumtazama Izaak

"Kumbe ndo maana" Alisema mtaalam

"Ndo maana nini?" Aliuliza binti

"Ndo maana mzee wako aliniambia kwamba nichunge kukuongelesha"

"Mh kwanini?" 

"Nahisi alijua sitaweza kuvumilia maana umewakaaaaa mpaka unatishaa"

"Mmmh" Mtoto aliguna kidogo

"Ndo hivyo nilipokuona tu moyo ukapiga paaaah lakini samahani nayoongea sijui ni nini naongea samahani sana" Alisema kijana Isaac maana alihisi anavuka mipaka

"Usijali jamani, kusifiwa mwenyewe napenda" Alisema Nuru

"Hahaaa, hapo sawa sasa....!" Jamaa alifurahi sana akaendelea kummwagia misifa mtoto wa watu, kama alikuwa na kilo 70 lazima zilifika 75 kwa sifa zile.

Safari yao iliishia Posta ambapo mzee alitaka kumfanyia surprise ya zawadi baada ya kuwa na matokeo mazuri ya chuo maana binti yule alikuwa ametoka kumaliza elimu ya Cheti katika chuo cha TIA 

"Hii ni zawadi yako mwanangu, hakika umenionyesha uwezo mkubwa kwa kiwango cha ufaulu wako Chuoni....hivi nilivyokupa ni hongera nataka leo pia tule bata kidogo mjini huku sio kujifunikia tu kule Mkoroshini Pangaboy sawa?" Alisema mzee kwa tabasamu.

Binti hakutaka kukagua hilo box lina nini ndani ila tu alishukuru na kupeleka kwenye gari.

Mzee yule alimchukua mwanaye na kwenda naye katika Hoteli ya kimataifa ya Kilimanjaro iliyoko pale Posta jijini Dar Es Salaam

"Baba" Alisema binti

"Naam?" Aliitika mzee

"Usinitumie tena kijana kama yule kuja kunichukua" 

"Kwanini?"

"Ana tamaa sana tena anataka kunitongoza mimi"

"Nini???" Mzee alifoka kwa hasira

"Ndio"

"Nilihisi atakutongoza tu na nilimpa onyo alipokuwa anatoka huku Shwaitani" alifoka mzee huyo na kuvuta menyu wakachagua chakula na kuendelea kupiga story mpaka kilipoletwa

Baadaye Kidogo mzee alitoka akiwa anaongea na simu akamuacha binti peke yake, binti hana hili wala lile, lakini mzee hakurudi zaidi ya nusu saa.

Nuru alichukua hatua ya kumpigia simu ili amuulize yuko wapi lakini mzee hakupokea, sasa kwa kuwa kabinti kalikuwa na kiburi sana, kaliinuka na kuondoka bila kuaga, hakumpa taarifa mtu yeyote, lakini malipo baba alikuwa ameshafanya

Hata hivyo kalitoka nje na kwenda kutazama gari ilipokuwa akaikosa binti, hivyo akajua baba hayupo karibu.

Hatua aliyochukua binti alitoka kabisa nje ya hoteli ile akapanda pikipiki mpaka stand.

Almashauri ya kichwa chake ilimuambia "Mh kwanini leo usitest utamu wa daladala?" ndipo binti akasogea kwenye daladala za Tegeta nyuki akakwea na kwenda moja kwa moja mpaka tegeta.

Alipofika tegeta mtoto wa kike hakusita, ilikuwa ni mida ya saa 4 usiku, daladala za Madale ni chache muda huo zilikuwa zimeshatokomea hivyo alifanya kupanda bajaji.

Bajaji ilitembea kwa mwendo wa madaa mpaka mkoroshini, ilikuwa na wateja wengine wa madale mwisho

"Nikuongezee sh ngapi unifikishe Pangaboy?" Aliuliza binti

"Mh hapana si unaona nina wateja wa madale mwisho, labda ushuke hapa uchukue pikipiki" Alisema dereva bajaji

Binti alifungua pochi akatoa noti ya 5000 na kumpa dereva, dereva alirudisha chenji 4000 halafu safari ikaendelea.

Binti alibaki kwa hasira pale chini huku akitaka kulia "Yaani mimi kweli baba ananiacha pale peke yangu? Lazima ameenda kumsaliti mama" Lilikuwa wazo la kwanza la binti huyo na kusogea nyuma

Sasa kwa mbali kabisa Side, Abiola pamoja na Noxy ambaye ni mwendesha boda walikuwa wameketi kijiweni, Side akamuona mtoto yule amesimama

"Oya Noxy nipe pikipiki chap nimpeleke yule demu man" Alisema huku akiinuka na kudandia pikipiki, Noxy akamtupia ufunguo na mshikaji akaiwasha chap na kumuwahi binti

"Hallo Nuru...." Alikosea hapo, binti aliposikia jina alishtuka maana alijua kabisa hakuna mtu anamfahamu pale, hivyo kutajwa tu ilibidi achunguze ni nani huyo anamuita.

Aliwasha mwanga wa simu na kummulikia, yaani Side alitabasamu mwenyewe "Nikupeleke Pangaboy sister?" Aliuliza Side 

"Hapana wewe sitaki labda bodaboda mwingine" Asee Nuru alimtolea nje sijui jamaa ana kisirani gani na manzi huyu.....ITAENDELEA

Sehemu ya 06
"Pumbaff" Kichwani Side aliwaza kwa hasira halafu akageuza pikipiki na kurudi pale alipokuwa Noxy pamoja na Abiola

"Vipi mzee, demu haendi?" aliuliza Noxy

"Daah tatizo eti pangaboy anataka kutoa 800" Alidanganya mshikaji ili asionekane kapigwa chini

Boda boda mwingine alimuwahi binti na kumchukua wakaondoka kuelekea huko kwa mtoto wa kike.

Alipofika nyumbani tu, Mama alikuja juu "Kwanini umekuja na pikipiki? baba yako yuko wapi?" Mama aliuliza

"Sijui, mi kaniacha hotelini zaidi ya saa zima halafu hapatikani sasa mimi nikae namsubiri mtu ambaye sijui kaenda wapi?" Alisema binti kwa hasira na kuingia chumbani halafu akarusha pochi

Mara baba naye akapiga, binti akaitoa simu alipotazama hivi baba ndo anapiga basi akasonya na kuendelea kuvua nguo zake ili aende kuoga. 

Baada ya dakika moja baba alipiga tena ndipo binti akapokea

"Wewe Nuru" Aliita mzee

"Nini??" Alimfokea baba yake

"uko wapi....umeenda wapi wewe? mbona nakupigia simu hupokei? enh"

"Niko nyumbani"

"Nyumbani?"

"Yah, yaani mimi ni wa kuniacha hotelini saa zima halafu wewe sijui umeenda wapi? Sasa we baba gani na simu ulizima"

"Oooh, I'm sorry mwanangu nilikuwa naenda ofisini kidogo"

"Haya nishafika nyumbani utanikuta"

"Sawa"

Mzee alikata simu akaegemea gari huku akiwaza itakuwaje kuhusu mkewe maana alikuwa ameshaharibu tayari.

Binti naye alioga.

**
Baadaye kwa Upande wa Side alikuwa amejilaza kitandani anawaza sana. "Ngoja mimi nikomae na Zakia ndo type yangu tena ntapata laki kutoka kwa Abiola kabisa" 

Alikuwa amejikatia tamaa kwa sababu alishajua yule mtoto wa mpemba kumpata sio rahisi hivyo kama alivyodhani. Aliendelea kulala mpaka asubuhi.

Mida ya saa mbili asubuhi Side aliamshwa na kelele za majirani wapangaji wenzake, ambapo aliamka na kutoa neti akalisokotea kule, halafu akashuka kitandani halafu akavuta suruali yake aliyokuwa amevaa jana.

Aliingiza mkono mfukoni na kukuta kuna noti kama tatu hivi za elfu kumi kumi na zingine ndogo ndogo.

Side alizichambua zile noti akatoa shilingi Elfu kumi kumi zile na kuweka kwenye begi lake kubwa, baada ya hapo alivaa ile suruali na kuinuka akachukua mswaki na dawa akatia.

"Daaah leo mbona nimeamka na njaa kali namna hii?" Alijiuliza mtaalam "Au kisa nilikula mapema jana" Aliwaza.

Alitoka nje na kuanza kuswaki huku mkono wa kushoto akiwa ameshikilia kikombe chenye maji.

Baada ya kuswaki alirudi ndani na kuvaa tishet halafu akaondoka na kwenda mtaani kutafuta hata chai au supu.

Alipofika njiani alikutana na wanawake watatu ambapo mmoja alikuwa ni Zakia, na wengine aliwakumbuka maana walikuwa wakifanya kazi kwa yule mpemba.

Side aliwapita bila hata salam lakini walianza shobo wenyewe "Ndo huyu" Walikuwa wakinong'onezana wanawake hawa
"Hamna sio huyu" Alisema dada mkubwa

"Mi nawaambia ndo mwenyewe" Zakia alidakia na kugeuka maana jamaa alikuwa ameshapishana nao tayari
"We kaka....." Zakia alianza kujileta mwenyewe "We kaka mwenye tisheti nyekundu" Alisema ndipo Side akageuka huku akijifanya anashangaa

Zakia alimuita kwa ishara ndipo Side akaweka mkono kifuani kumuuliza kama ndo yeye anamuita

"Ndio ni wewe" Alosema Zakia

"Mh" Side aliongea huku akirudi nyuma na kuwasogelea 

"Mambo" Zakia alianza

"Safi...vipi?"

"Pouwaa,, samahani hivi wewe ndo ulileta viatu pale kwa mpemba siku ile?" Aliuliza

"ndio mimi......vipi..."

"Sasa je!! Si nilisema?" Alisema Zakia huku akiwageukia wenzake

"Haya bana mbona haujagi tena?"

"Ntakuja ila pale panaogopesha" Alisema mtaalam

"Kweli najua, ila....karibu sana"

"Asante but.....mmetoka wap?" aliuliza

"Sokoni"

"Asubuhi hii?" aliuliza

"Ndio"

"Poa..." Side alisema na kutoa kitochi mfukoni akaanza kukibonyeza bonyeza na kumkabidhi Zakia hata bila kumuambia chochote, ndipo Zaki akajiongeza akachora namba yake na kuagana

"Basi tutachat" Alisema binti

"Poa"

Side alipoondoka pale kwanza hakuamini kile alichokuwa amekiona, alichekelea mwenyewe yaani maana hakujua angeipata namba kirahisi namna ile.

Alisonga mbele mpaka Hotelini, hata hivyo ilikuwa ni jumapili Abiola hakwenda kazini maana alikuwa akifanya kazi serikalini

"Niajeeee" Side alisema kwa furaha huku akimpa tano Abiola halafu akaketi pembezoni

"Lah!! Ni guudi"

"Ok mama niletee Supu na chapati mbili huko" Alisema huku akichomoa simu mfukoni na kumuonyeshea namba ile Abiola "Namba hii hapa, ninamaliza mchezo soon andaa laki yanguuu" alisema mtaalam

"Nimemuoana kapita hapa na wenzake, mzee ukifanikiwa pale nakupa laki manina" Alisema mtaalam

"Haya poa tena ngoja nimtext now" Alisema Side na kuanza kuandika message ili amtumie Zakia......ITAENDELEA....JE SIDE ATAFANIKIWA KWA ZAKIA?
Soma mpaka mwisho kwa sh 1000

Previous Post Next Post