1-----5
NIWEWE PEKEAKO .
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU 1.
BOOKING 0743433005 .
Katikati ya jiji la Dar es salaam , jiji la mishemishe lilo jaa kila aina ya vishawishi na starehe mbalimbali. Maeneo ya Kinondóni mkwajuni kuna binti moja anaitwa Miriam. Miriam ni binti mwenye miaka 20 tu ni mzaliwa wa hapo hapo Kinondóni mkwajuni.
Maisha ya Miriam ni yakawaida sana. Alikuwa akiishi yeye na mama aké ambaye ni mlemavu wa miguu . Miriam yeye alikuwa akimuhudumia mama aké tangia ana miaka 10 tu . Miriam alikuwa akiuuza makopo ili mama aké aweze kula uku akisaidiana wanasalia wema kumuhudumia mama aké huyo.
Baba Miriam alimteleka mkewe baada ya kuwa na mimba ya Miriam ndipo alimkimbia mke wake. SÃ babu mke alikuwa mzima aliona nitalea mwenyewe mtoto wangu . Alianza kufanya vibarua kama kulima bustani na kufua nguo kwa watu ili apate maitaji .
Adi mimba ilipofika muda wa kujifungua . Mama Miriam alijifungua mtoto wa kike ndio Miriam. Mama Miriam alimlea binti aké kishida shida adi alipofikisha miaka ya kuenda shule. Miriam alianza shule ya msingi uku mama akifanya kà zi zilezile ili kumlea mwanae adi Miriam alipofikisha miaka kumi na kuingia darasa la tatu.
Siku moja mama Miriam akiwa anarudi nyumbani kwake kutoka kwenye kà zi zake za kumpatia ridhiki ili aweze kula yeye na mwanae. Kipindi yupo barabarani ambayo sio ya rami ni ya vumbi ila imewekwa vizuri magari na boda uwa zinapita hapo. Mama Miriam alikuwa yupo busy akiongea na simu na mteja wake.
" Nimekwambia kesho nitakuja kukufuria wala usijali" . Uku akiwa anavuka barabara bira kuangalia pambeni ghafra gari ndogo ilikuwa inakuja kwa speed na kuonga mama Miriam. Mama Miriam alidondoka chini na simu ilidondoka chini palepale.
Mwenye gari baada ya kuona watu wanakuja alibidi akimbie kwa ajiri ya usalama wake. Wà salia wema walimchukua mama Miriam na kumpeleka hóspitali kwa ajiri ya matatibu. Walimfikisha hospital vizuri tu na kumuita daktari kwa ajiri ya matatibu.
*********************
Daktari alibidi aende muangalia mgonjwa na kukuta miguu aitamiki. Daktari alibidi atoke nje tu. Watu waliompeleka sababu walikuwa wanamjua mama Miriam alipogogwa ni maeneo anapoishi walibidi wamfate daktari.
Daktari aliwarudisha na kuwaomba watu wa wawili wazima. Watu wengi walijua mama Miriam amefariki dunia kila moja alibakia kujiinamia na kutafakari itakuwaje kuhusu Miriam. Wale watu waliingia kwa daktari .
Daktari aliuliza'' huyu mgonjwa ni nani yenu ? Wale wazee wajibu " huyu mgonjwa tunakaa naye mtaani aligongwa na gari kipindi anarudi nyumbani kwake". Daktari aliuliza'' ana ndugu yóyote yule? Wale wazee walijibu " ndugu atujawahi kuwaona ila alikuwa anaishi na mwanaume kama mume wake ambaye alikuwa anafanya kà zi migodini baada ya kufanikiwa alimuacha mke wake akiwà mjamzito na kwenda kuoa".
" Kwa kifupi ana mtu yóyote yule tunayemjua sisi zaidi ya mwanae ambaye ana miaka miaka kumi tu ". Daktari " ooooh poleni sana mgonjwa wenu nà mzima wa afya sema ana changamoto kidogo ". Wazee walitabasamu nakuuliza " changamoto ipi daktari?
Daktari alijibu " anatakiwa afanyiwe operation ya kukatwa miguu yote miliwi ndio ili aliaribika " . Wazee walishtuka kidogo na kuangaliana . Daktari aliwambia" ndio hivyo ilà ina bidi mchangie laki mója". Wale wazee walijibu " sà wa " kutoka nje.
Walitoka nje bahati nzuri walikutana na mwenye kiti wao na mjumbe wake . Wale wazee walibidi waseme walichoambiwa na Daktari. Watu waliumia sana na kuchangishana vizuri adi kupata laki mója kumpa daktari.
Madaktari na manesi majira ya sà a kumi walimuingiza fieta na kumkata miguu yote miwili ambayo inashida na kuwa ana miguu. Miriam kipindi chote cha tukio alikuwa yupo shuleni kipindi anarudi nyumbani kwao yupo njiani. Alipishiña na mke wa mjumbe wa nyumba kumi.
Miriam alimsalimia " shikamoo mama" . Mke wa mjumbe aliitikia" marhaba ujambo" na kumuita . Miriam alibidi aende adi pale . Mke wa mjumbe aliingia ndani na kumpa chakula.
je nini kitatokea.
itaendeleaa
NIWEWE PEKEAKO .
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU 2.
BOOKING 0743433005 .
Miriam alikataa kula nakusema" nimeshiba " na kutakuondoka . Mke wa mjumbe alimzuia nakumwambia " usiende". Kidogo mjumbe ana rudi nyumbani kwake na kumkuta mke wake na Miriam. Mama mjumbe aliuliza'' kwema uko ?
Mjumbe alijibu" hali ya mgonjwa sio mzuri mama Miriam amekatwa miguu yote miwili " . Miriam alishtuka" nini mama angu amekatwa miguu ? Mjumbe na mkewe walibidi waangaliane mjumbe alibidi amwambie ukweli .
" Ndio mama ako amekatwa miguu yupo hospital"..
Miriam alilia kama mtu mzima masikini. Mjumbe alisema" kwahiyo utakaa kwangu adi mama ako atakapo ruhusiwa hospital". Miriam alijibu kinyonge " sawa ". Alibidi aende nyumbani kwao kuchukua nguo zake yeye na mke wa mjumbe .
Walifika ndani kwa kina Miriam mke wa mjumbe alibakia kushangaa ! japo mama Miriam ni single mother lakina chumba ni kizuri kwani alibarikiwa chumba na sebure ni nyumba aliyoijenga yeye na mume wake. Mke wa mjumbe alimsaidia kutoa nguo zake yeye na mama ake za kumpelekea hospitali na kisha kufunga nyumba kutoka .
Walirudi kwa mjumbe na kuingiza mizigo ndani kisha yeye kutoka nje kuendelea na kupika chakula cha usiku. Mke wa mjumbe alisema" kesho asubuhi inabidi niende hospital". Miriam alisema " na mimi naenda kumuangalia mama angu ". Mke wa mjumbe alijibu " sawa".
Mke wa mjumbe na Miriam walipika na kukaa kula. Mke wa mjumbe tangia aolewe na mjumbe akuwahi kumpata mtoto ata moja japo mjumbe alikuwa na watoto wakubwa tu 3. Mke wa mjumbe kwa vile alikuwa anashida ya mtoto tangia miaka kumi ya ndoa yake akupata mtoto alitokea kumpenda binti Miriam tangia mdogo .
Hivyo sikuhiyo alikuwa ana furaha kupewa kukaa nae ukizingatia mtoto mwényewe ni anaheshima sana . Walimaliza kazi zao na kuingia ndani wakiwa wanafuraha japo Miriam alikuwa anafuraha. Mke wa mjumbe alitenga chakula yeye na Miriam na kukaa kula kuelekea kulala.
**********************
Hospitali ya Mwananyamara ambapo amelazwa mama Miriam. Majira ya usiku sà a nane mama Miriam alikuwa amelala kutokana na alipoteza fahamu . Mama Miriam alianza kuweweseka kwenye ndoto kuwa kuna mtu mrefu alikuja na kutaka kumuua .
Mama Miriam alikuwa akipambana na huyo mtu ili asimue na kutetea uhai wake. Kipindi anagombana na huyo mtu kuokoa maisha yake uku akipiga makelele kwenye ndoto . Madaktari walikuwa wamejazana kitandani wakimuangalia mama Miriam mapigo yake ya moyo yanaenda kwa kasi zaidi .
Mama Miriam aliendelea kugombana na yule mtu . Yule mtu ambaye kaficha uso wake alichofanya yeye alimkata miguu yote miwili. Mama Miriam alipiga kelele nyingi kwa uchungu adi Madaktari walishangaa ! mama Miriam alishtuka hapohapo usingizi.
Alibaki kushangaa ! mà ana aelewi elewi nakutaka kukimbia Madaktari walimuai na kumshika sababu akuwa na miguu. Mama Miriam alitaka kusimama masikini aliona awezi . Madaktari walibakia kumuangalia tu na kimuonea huruma .
Daktari moja alibidi amwambie ukweli " pole mama kuanzia leo uwezi kutembea tena auna miguu ". Mama Miriam aliuliza'' nini ? Alifunua shuka na kukuta ana miguu kweli. Alibidi anze kulia na kupigana kelee uku akimtaja Múngu.
Madaktari kwa vile waliona kelele zinakuwa nyingi na kuamua kumpiga sindano ya usingizi ili asisumbue wagonjwa wengÃne . Mama Miriam pale pale alilala tena masikini . Daktari alimfunika na kutoka nje kwenda ofisini kwao .
Asubuhi na mapema mke wa mjumbe na Miriam waliamka na kupika uji kumpelekea mgonjwa hospital . Mke wa mjumbe na Miriam walichukuana adi hospital bahati nzuri sababu ya Mama Miriam kuishi na Watu vizuri walikutana na majirani zake wa wili nao wamebeba uji .
Miriam aliwasalimia vizuri yeye na mke wa mjumbe nakuingia hodini wote . Walimkuta mama Miriam amelala kitandani tu . Miriam aliingia na kumuangalia mama aké machozi yalimtoka akiwà amemfunua shuka lake. Miriam kipindi machozi yanamtoka yalimwagikia mama aké na mama aké aliamka.
itaendeleaa.
NIWEWE PEKEAKO .
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU 3.
BOOKING 0743433005 .
Mama Miriam alishtuka nakuanza kulia masikini ya Múngu uku akimuangalia binti yake . Miriam nae uvumilivu ulishindwa na kuanza kulia kwasauti . Mke wa mjumbe alibidi ambembeleze Miriam anyamaze . " Miriam nyamaza mama ale sà wa ".
Miriam alijitaidi kunyamaza lkn ilishindika masikini aliendelea kulia . Mama Miriam nae alibidi ache kula nae nakuanza kulia. Walilia mtu na mama aké wakiwa wamekumbatia . Manesi walipita nakusema" muda wa kuangalia mgonjwa umekwisha".
Mke wa mjumbe na wezake walibidi wajitaarishe kutoka nje. Mama Miriam na Miriam walikuwa wamekumbatia wakilia masikini. Mke wa mjumbe alimwambia " Miriam umesikia muda wa kuangalia mgonjwa umekwisha ". Miriam ndio alizidi kumkubalia mama aké kwa nguvu.
Watu wote walitoka hospital kasoro wakina Miriam tu . Mke wa mjumbe alijitaidi kumtoa Miriam ilishindikana. Nesi mója aliingia hodi na kuwakuta " nyie vipi amjasikia tangazo au ? Mke wa mjumbe alijibu " tumesikia sema huyu mtoto ataki kumuachia mama aké".
Nesi alÃuliza" mtakujaje na mtoto hospital ingawa mnajua mtata ? Mke wa mjumbe alibakia kimya kasimama . Nesi alitoka na kuelekea nje kumuita vijana waskauti . Vijana wa waskauti na nesi waliingia hodini. Nesi alisema" mtoeni huyu mtoto nje daktari anakuja ".
Vijana wa skauti walimtoa kinguvu uku Miriam akiwa analia sana masikini . " Niacheni nibaki na mama angu mie jamani ". Walimbeba adi nje na kumpa mke wa mjumbe mtoto. Hodini Mama Miriam alilia kwa uchungu masikini akikumbuka shida alizopata yeye na binti ake adi kufika hapo na leo hii ana miguu alilia sana.
Mama Miriam alibakia kumshukuru Múngu tu kwa kila jambo masikini . Alibidi aendelee kulala akiwà na uzuni . Miriam na mke wa mjumbe walibanda majaji warudi kwao . Miriam akiwa yupo kwenye uzuni sana. Mke wa mjumbe walimkumbatia " usijari mama atakuwa sawa muombee Mungu tu .
********************
Miriam aliitikia kwa kichwa na kuendelea kumlalia mke wa mjumbe miguu. Safari iliendelea adi kufika kwao walishuka mke wa mjumbe alilipia vizúri na kuingia ndani . Walifika sebreni na kukuta mjumbe na binti aké ambaye anaitwa Zai na mtoto wa kiume anaitwa Abuuh.
Mke wa mjumbe alishangaa! baada ya kuwaona watoto wa Mume wake . Alibidi awafate kwa furaha na kutaka kumkumbatia Zai. Zai alichofanya alimkwepesha mama aké wa kambo na kumshusha juu adi chini na kumfonya.
Mke wa mjumbe alijisikia vibaya sema alijikaza nakuwauliza " umekuja sà a ngapi ? Abuuh alijibu'' ungekuwa unataka kujua tumekuja sà a ngapi hapa nyumbani usingenda kuzurula muda wote ". Miriam alijisikia vibaya na kuingia ndani masikini akiwa amekaka kitandani .
Mke wa mjumbe alimfata ndani ukouko .Nje watoto wamjumbe wakiwa wanamcheka mama yao wakambo . Mjumbe aliingilia kati" ebu keleleni alafu muwe na adabu na heshima mjue yule ni mama yenu ". Abuuh na dada aké walicheka sana kwa nguvu .
" Eti mama yetu huyu mama yetu ulimfukuza kama mbwa sà babu ya huyu mwanamke wakó ". Abuuh alienda kusema " mama yetu gani ambaye kasababisha mama yetu atoke nyumbani" . " Huyu ni malaya kama malaya wéngine".
Mjumbe alishikwa na hasira na kumpiga kofi mwanae " Abuuh kuwa na adabu mwanangu ". Abuuh " baba unanipiga mimi sà babu ya huyu malaya wako ok sawa". Alichukua simu yake na kuondoka zake ndani uku dada aké nae akiwà mbali alimfata .
Waliingia chumbani kwa pamoja na kuanza kucheka . Zai alisema'' Abuuh nakubari tumfanyie vituko adi aondoke tu kwanza anajaza mitoto tu umu ndani. Abuuh alijibu'' usijari atakotoka tu umu ndani yeye na mtoto wake". Miriam baada ya kuona aelewi elewi aliingia chumbani kwake na kutoa nguo kutoka kuondoka kurudi kwao.
Mke wa mjumbe alimzuia " unataka kuondoka kwenda wapi Miriam ingawa mama ako yupo hospital? Miriam alijibu'' siwezi kukubari uteseke sà babu yangu mimi niache niondoke tu " .
Itaendealeaa.
NIWEWE PEKEAKO .
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU 4
BOOKING 0743433005 .
Mke wa mjumbe alimshika mkono na kumkumbatia nakusema" ukuja sà babu yangu mwanangu ulikuja sà babu ya mjumbe ndio aliyekureta hapa ". Aliendelea kusema " kwahiyo baki kwa niaba ya mjumbe ilikulinda heshima yake ". Miriam alijikuta akili sana masikini akiangalia mama aké mgonjwa aliyemsaidia ana matatizo nae alilia sana.
Mke wa mjumbe alimbembeleza sana na abakie masikini . Miriam alimkumbatia mke wa mjumbe masikini . Mke wa mjumbe alifurahi na kufuta machozi . Wakiwa wamekumbatia ghafla mlango ulifunguliwa kwa nguvu .
Mke wa mjumbe alishtuka na kuangalia nani aliyefungua mlango hivyo alimkuta mtoto wa mjumbe Zai. Zai aliwaangalia juu adi chini na kufonya " yani nyie mmekaa ndani tu bora mkapike sisi njaa inauma ". Mke wa mjumbe alibidi amuangalie tu nakumuacha .
Zai alijidahi kumuita kaka aké" Abuuh , Abuuh , Abuuh awa vijakazi bora wakapike wamekumbatia tu". Abuuh alibidi aende adi pale na mke wa mjumbe na Miriam walibidi watoke nje . Zai na Abuuh walibakia kucheka na kutoka kwenda kucheza kalata .
Mke wa mjumbe na Miriam waliingia jikoni na kupika chakula vizuri uku Miriam mtoto wa darasa la tatu akimsaida . Walimaliza kumpika na kutenga chakula mezani. Zai alikuwa yupo form three na Abuuh kamaliza form 4 kafeli yupo gereji .
Walikuwa wapo busy wakicheza kalata Zai na kaka aké wezake wakitenga chakula. Baba yao aliingia ndani na kuwakuta watoto wake wakichezea kalata uku wezao wakitenga chakula. Aliwaangalia na kubakia kusikitika kuingia ndani kwake tu. Mkewe alÃbidi amfate ndani nakumwambia" chakula teali ".
Mjumbe na Mkewe walitoka nje na kwenda kula walishaanga! kuwaona wamekaa wanakula mtoto wamemuacha amekaa. Mjumbe uvumilivu ulimshinda aliwauliza " hivi nyie amuoni alibu au ? Aliendelea kusema" mtoto wa watu kawatengea vizuri chakula mnakula bira kumuita".
Zai alijibu'' house girl alipamoja na mabwana zake , house girl anakula makombo tu". Mjumbe alishikwa na hasira na kutaka kumpiga mwanae. Miriam alimdaka mkono " mjumbe msamehe bure usimpige kwa jiri yangu ni sawa yupo sahii mimi ni wakupita tu hapa ndani na yeye ni wakudumu. Mjumbe alijisikia vibaya sema alijikaza na kuendelea kukaa zake .
*********************
Mke wa mjumbe alimpakulia chakula mume wake na Miriam . Miriam alifumba macho na kusali masikini ya Mungu . Watu wote walibaki kumuangalia tu. Mjumbe alisema" angalia watoto wawezenu walivyo lelewa kwenye maadili mema ". Kile kitendo Zai kilimkasirisha nakujisema " nitamkomesha ".
Miriam alimaliza kusali na kuangalia watu wote wanamuangalia yeye . Akujali aliendelea kula masikini ya Mungu. Walikula lkn Zai sababu ni mvivu alikula alaka alaka akwepe kutoa viombo . Alimaliza kula na kutoka meza kwenda kukaa pembeni.
Watu wote walimaliza kula Miriam alitaka kukusaya viombo . Mjumbe alisema" acha atakusanya Zai". Zai " lakini baba kwani mimi ndio wa mwisho ? Mjumbe alisema'' nimesema hivi kusaya vyombo na ukaoshe sitaki ujinga nyumbani kwangu ". Zai alishikwa na hasira nakutoka mkuta Miriam amesimama alimpiga kipensi kwa asira na kutoa vyombo kwenda kuosha.
Walienda kulala zao wenyewe japo Miriam akuwa sawa akiangalia ajui atima ya mama aké. Hospital mama Miriam alikuwa akianza mazoezi rasmi na kutembelea baskeli za walemavu walikuwa wamekatwa miguu. Alijikuta akilia tu masikini ya Mungu na kumlani Mungu kwanini kampa matatizo anajua shida yake.
Mama Miriam alilia sana akiangalia yeye ndio baba na yeye ndio mama kwa binti aké alafu amekatwa miguu yote miwili . Alijitaidi kufanya mazoezi masikini ya Mungu lakini alishindwa na kuamua kukaa kulia tu akifikilia. Akiwà amekaa ghafla mlango ulifunguliwa na kuangalia kumkuta mama Musa na mmama mója mnene ambaye wamekuja hospital.
Mama Musa ambaye jirani yake alimletea chai masikini na vitumbua . Mama Miriam alishukuru "asantee sana ndugu zà ngu ". Mama Musa alijibu'' usijari swaiba kuwa huru ". Mama Miriam alikaa kimya masikini na kuwangalia .
Yule mmama alipiga magoti nakusema " naomba unisamehe mimi ndio niliyekugonga nakuomba unisamehe sana ". Mama Miriam alijibu'' wala usijali aya yote ni mapenzi ya Mungu ". Yule mmama alijisikia vibaya sana kuita nesi alipe biri angalau achangie kidogo matibabu .
Nesi alimpa biri yule mama alilipia na kuondoka zake masikini akiwa na uzuni . Mama Miriam alibakia hospital tu akiwà na uzuni nae masikini . Nyumbani kwa mjumbe Miriam aliamka vizuri ilikuwa jumapili alikuwa akifagia uwanja mwenyewe . Zai alikuwa anachukua takataka na kurudisha.
itaendeleaa.
NIWEWE PEKEAKO .
MTUNZI BEBAS CUTELY .
SEHEMU 5.
BOOKING 0743433005 .
Miriam " lakini nini mbona unanifanyia hivyo ? Zai alimuangalia juu adi chini nakutaka kuongea ghafra mlango unafungulia baba aké anatoka . Miriam alimuona mjumbe na kumpigia magoti " shikamoo". Zai alishtuka baada ya kumuona baba aké kaja na kuangalia chini .
Baba Zai alÃuliza " vipi kunanini ? Miriam na Zai walibakia kimya kumuangalia tu baba yao . Baba Zai alimuuliza mwanae " wewe mbona umekaa tu unashindwa na mtoto anafagia Kweli ?
Zai alibakia kimya anaunyaunya tu pale. Baba Zai alisema'' sijúi mama enu kawaleaje watoto wangu yan kanialibia watoto kabisa mama yule mwingine mvuta bangi wewe nae mvivu ". Miriam alióna aibu masikini nakupiga magoti " bamjumbe msamehe ".
Baba Zai alimuangalia binti Miriam nakumnyanyua " usijari mwanangu nimemsamehe" . Miriam alijibu'' asantee bamjembe . Baba Zai alimuangalia mwanae juu adi chini nakumwambia" potea hapa nisije kukupiga bure ":Zai aliona aibu nakukimbia uku akiwa analia kama vile mtu kaonewa vile .
Aliingilia ndani nakujisemea " Miriam utakoma adi utoke nyumbani kwetu ". Aliendelea kusema" aiwezekani kila kitu usifiwe wewe tu siwezi kukubari" . Miriam uku nje aliendelea na kazi yake kufagia mwenyewe. Alimaliza kufagia na kuingia ndani mwenyewe.
Mke wa mjumbe alikuwa ayupo ameenda hospital kumuangalia mama Miriam . Zai baada ya kusemwa sà babu ya Miriam alichofanya alikula vitafunio vyote na chai kwenda kumwaga . Miriam alimaliza kazi na kwenda kuoga kuvaa nguo safi kutoka na kwenda sehemu ya kunywa chai .
Miriam alishangaa! akukuta chai masikini ambayo mke wa mjumbe alimuwekea yeye na Zai . Alibidi atoke mezani na kuingia ndani akiwa kapoa . Zai alikuwa yupo busy kucheka maana alikuwa ayupo mbali . " Uoni aibu kutaka kula mbele ya boss wakó .
Aliendelea kusema" wewe ni house girl kazi yakó ni kufanya kà zi tu na kusifiwa kula tuachie sisi". Miriam alimuangalia na kuingia ndani masikini ya Mungu na kulia tu kumkumbuka mama aké hospital. Zai alibakia kumcheka mwenziwe bà si .
*******************
Mke wa mjumbe alikuwa yupo hospital kwenda kumuangalia mama Miriam. Mama Miriam alimuuliza" mwanangu ajambo? Mke wa mjumbe alijibu'' ajambo yupo ". Mama Miriam" sà wa kama yupo salama". Aliendelea " nikuombe kitu ?
Mke wa mjumbe" yes niombe " . Mama Miriam alisema'' naomba unilindie mwanangu". Mke wa mjumbe alijibu" usijali ". Mama Miriam alisema'' nipo chini ya miguu yakó naomba unilindie mwanangu ". Mke wa mjumbe alijibu'' usijari mwanao yupo mikono salama ". Mama Miriam alijibu'' sawa .
Mke wa jumbe alimuaga na kuondoka zake nyumbani kwake . Alifika nyumbani kwake na kuingia ndani kukuta ugomvi . Zai alimkuta Miriam kalala njaa inamuuma kaenda kumwagia maji mwezake . Miriam akukubari nae kaenda kumwagia maji na yeye .
Zai alimfata mwezake na kumpiga na mweziwe akukubari alimpigia nae . Ndio ugomvi ulipokuwa mkubwa sana . Mke wa mjumbe aliingia ndani nakuuliza " nyie nini mnapigana ? Miriam alijibu akiwà analia " da Zai kanikuta nimelala kanimwagia maji ".
Zai " wewe koma acha kunisingizia upó eeeh". Mke wa mjumbe alimgeukia " hivi Zai utakuwa hivi adi lini mwanangu wewe eeeh ? Aliendelea " mbona baba enu anatabia hiyo roho mbaya nyie mmefata kwanani? Zai kujitia kulia kama kaonewa.
Kidogo kaka aké aliingia ndani na kumkuta mdogo wake analia . Abuuh alimkata jicho mama ake wa kambo nakuuliza" kuna shida gani hapa ? Mke wa mjumbe alijibu'' mdogo wako kampiga mtoto watu na mkanya ndio analia ". Abuuh aliuliza "' una mkanya wewe kama nani umemzaa huyu ?. Mke wa mjumbe alibakia kimya .
Abuuh alimpiga singi mama aké wa kambo nakumwambia" hebu punguza kieleele kama umeoga nje ". Alimsukuma na kumchukua mdogo wake kuingia ndani.
Tags
Simulizi