Kama umeiona hotel rwanda bas nakuletea nyingine hii ambayo nayo ni true story , inazungumzia kipindi hicho hicho cha vita ya kikabila kati ya wahutu na watutsi nchini rwanda .
Kulikuwepo na shule ya kanisa ambayo ndani yake kulikua na kanisa pamoja na kambi ya jeshi la umoja wa mataifa , wakati wa operation ya wahutu kuchinja chinja watutsi ambao ni wachache kushinda wahutu nchini rwanda , mamia ya watutsi walikimbilia hapo shule .
Ni eneo salama kwa 7bu ya uwepo wa jeshi la umoja wa mataifa , hata wanamgambo wa wahutu walishindwa kuingia kwa kuheshimu jeshi la umoja wa mataifa .
Walibaki nje tu ya fensi wakisubiri jeshi liondoke na raia wa kizungu ili wao waende kuwaua watutsi waliopo hapo shule , hata wanajeshi wa umoja wa mataifa walishindwa kufanya kitu zaidi ya kulinda tu 7bu kisiasa inaweza kua jambo lingine kimataifa .
Kikawaida ktk majanga kama hayo mataifa ya kizungu yana tabia ya kuwaondoa raia wao tu ktk nchi za namna hiyo , kwa hiyo hata hapo pia yalitumwa magari kuwachukua raia wageni kuwaondosha hapo nchini .
Magari hayo yalisimamiwa na jeshi kuwachukua wazungu tu na kuwaacha waafrica , haijalishi hata kama mtoto mchanga hauchukuliwi maana inaweza kuleta shida .
Wapo wazungu walioumia kuondoka huku wakiwaacha waafrica waliowazoea , kusubiri kuchinjwa na waafrica wenzao .
Hawakua na budi maana wakisema wakae na wao watauliwa , hatimae walichukuliwa na hata jeshi nalo liliondoka likiwaacha watutsi wapambane na hali yao wenyewe .
Kuna padre mmoja wa kizungu ambaye ndo aliyekua akisalisha ktk kanisa la hapo , yeye alikataa kuondoka .
Aliona abaki tu na kama kufa atakufa nao hao waafrica , kwa kuwa jeshi lilishaondoka bas ikawa fungulia mbwa kwa wahutu .
Shida ni kwa hao waliobaki kutoka hapo salama
Ni Moja kati ya muvi kali za africa
Enjoy 🙏
Kuipata movie hii na nyingine kibao za namna hii bonyeza hapa Download movie hii
Tags
movies